Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, March 30, 2015

PICHA::Matembezi ya hamasa kupiga vita mauaji ya Albino "Imetosha"


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe na Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr wakiongoza matembezi ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam kuanzia viwanja vya Biafra mpaka Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.
DSC_0573
DSCF7252
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar 

 
Kweigyr, Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu, Mwakilishi wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Abdillah Omar sambamaba na wadau wengine wakishiriki kuimba wimbo ‘Tanzania Tanzania’ kabla ya kuanza kwa shughuli nzima ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika jana kwenye viwanja vya  Leaders Club, jijini Dar es salaam.
MMGL2036
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr akicheza muziki wa sambamba na Mwanamuziki wa Reggae, Jhiko Manyika “Jhikoman” wakati wa shughuli nzima ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar  es salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network ambao ni wadau wakubwa wa harakati ya Imetosha, Joachim  Mushi.
MMGL2290
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Matembezi ya Hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini (Imetosha), Ally Masoud “Kipanya” akimkaribisha Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu ili kuzungumza na Watanzania waliofika kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.
MMGL2338
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akitoa hotuba yake na kauli ya Serikali katika harakati ya kupambana na kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment