Katika gazeti la Taifa Imara la tarehe 23 Machi 2015 kulikuwa na habari
yenye kichwa cha maneno ' Zitto amchongea Mengi kwa JK?' Habari hiyo
ilibeba maudhui ya 'post' iliyoandikwa katika mtandao wa Mwanahalisi
online.
Habari hiyo inaonyesha kuwa Mimi nilikutana na Rais kwa msaada wa watu
mbalimbali na katika kikao hicho inadaiwa nilisema kuwa Mengi ndiye
aliyechochea wabunge kuishughikia Serikali ya Rais Kikwete ili ianguke.
aliyechochea wabunge kuishughikia Serikali ya Rais Kikwete ili ianguke.
Ni vema ifahamike kuwa gazeti la Taifa Imara linamilikiwa na Bwana James
Rugemalira wa kashfa ya Escrow na kuendeshwa na Bwana Prince Bagenda
aliye organise press conference ya mmoja wa mawaziri waliofukuzwa kazi
kwa kashfa hiyo. Vile vile chanzo cha habari hiyo ni mtandao wa
mwanahalisi online ambao unaendeshwa mmiliki wa Mawio gazeti ambalo kila
wiki lina habari za kutunga dhidi yangu na chama cha ACT Wazalendo.
Habari hiyo ni ya kutunga yenye fitna zenye lengo la kuchonganisha watu. Naomba kufafanua ifuatavyo
1 Taarifa Maalumu ya Kamati ya PAC kuhusu ufisadi wa tshs 306 bilioni za
Escrow hauhusiki na Bwana Reginald Mengi kwa namna yeyote ile. Mengi
sio mbunge, sio mjumbe wa PAC na hakushawishi PAC kwa namna yeyote ile.
Wezi wa Escrow wasitapetape kutafuta mchawi wakati mchawi ni wizi wao
wenyewe. Porojo za kwamba Mengi alihonga wabunge ili kuishughulikia
Serikali zinabaki porojo tu. Ila kama kuna mtu ana chembe ya ushahidi wa
jambo hilo apeleke kwenye vyombo vya dola kwa hatua kuliko kurudia
rudia porojo hizo kwenye vyombo vya habari.
2 Sihitaji kutumia watu ili kukutana na Rais Jakaya Kikwete kwani
ninaweza kukutana naye kwa taratibu za kawaida kabisa za kiserikali.
Hadithi ya kwamba nimeomba watu wanikutanishe na Rais inaonyesha namna
mwandishi alivyoshindwa kutunga uongo wake. Katika kukutana kwangu na
Rais kikazi sijawahi hata mara moja kuzungumzia watu. Hivyo kusema
nilikwenda Ikulu kumzungumzia Bwana Mengi ni kunidharau na kuidhalilisha
Taasisi ya Urais.
3 Nimemwelekeza mwanasheria wangu achukue hatua za kisheria dhidi ya
Gazeti la Taifa Imara na vilevile Gazeti la Mawio kwa mfululizo wa
habari za kutunga uongo dhidi yangu kila kukicha. Nimeagiza tupeleke
mashtaka kwenda Baraza la Habari Tanzania ili magazeti hayo yathibitishe
habari zao.
Zitto Kabwe
Kiongozi wa ACT Wazalendo
No comments:
Post a Comment