MCHEZA sinema maarufu duniani wa Marekani, Sylvester
Stallone ‘Rambo’ amesema bondia Floyd Mayweather atashinda katika pambano dhidi
ya bondia Mfilipino, Manny Pacquiao litakalofanyika Mei 2 mwaka huu.
Mcheza sinema maarufu duniani Sylvester Stallone 'Rambo' na
bondia Manny Pacquiao.
Hata hivyo, mtangazaji wa mapambano ya ngumi, Larry
Merchant, alitofautiana na Rambo aliposema kwamba yeye anaweka kete zake kwa
Pacquiao kushinda pambano hilo.
Pambano hilo ambalo ndiyo ‘gumzo la mjini’ limeonyesha pia
kwamba bondia maarufu wa zamani, Muhammad Ali, amesema mshindi atakuwa
Pacquiao. Hii ni kwa mujibu wa binti yake aliyewaambia waandishi wa habari.
Binti huyo, Laila, naye ni bondia Mmarekani ambaye alistaafu bila kushindwa.
CHANZO: MTANDAO WA PULSE>NING
No comments:
Post a Comment