Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, April 9, 2015

TANZANIA YADONDOKEA KUNDI LA KIFO AFCON

Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa mwaka 2017 imepangiwa makundi yake ya michuano ya kufuzu hii leo (jumatano) huko Cairo nchini Misri kwenye makao makuu ya shirikisho la soka barani Afrika CAF .
Makundi hayo yaneshuhudia timu kubwa zikipangwa kwenye nafasi za kwanza huku zikipangwa na mataifa madogo kama ulivyo utaratibu wa kugawa nafasi kuendana na viwango vya ubora.

 
Timu ya taifa ya Tanzania imepangwa kwenye Kundi G ambako inaambatana na timu za taifa za Misri , Nigeria na Chad .


Makundi hayo ni kama ifuatavyo.
Kundi A ; Tunisia , Togo , Liberia , Djibouti . Kundi B ; Congo Drc , Angola , CAR , Madagascar.
Kundi C Mali , Equatorial Guinea , Benin , South Sudan. Kundi D; Burkina Faso ,Uganda , Botswana , Comoros.
Kundi E; Zambia , Congo , Kenya , Guinea-Bissau. Kundi F ; Cape Verde , Morocco , Libya, Sao Tome.
Kundi G; Nigeria , Egypt , Tanzania , Chad. Kundi H; Ghana , Mozambique , Rwanda , Mauritius.
Kundi I ; Ivory Coast , Sudan , Sierra Leone , Gabon . Kundi J; Algeria , Ethiopia , Lesotho , Seychelles.
Kundi K ; Senegal , Niger , Namibia , Burundi . Kundi L ; Guinea , Malawi , Zimbabwe , Swaziland.
Kundi M ; Cameroon , South Africa , Gambia , Mauritania .
Michezo ya kufuzu kwa makundi haya itaanza kupigwa mwezi juni mwaka huu ikiendelea mpaka mwakani .
Washindi wa makundi haya na timu mbili zilizomaliza hatua hii kwa rekodi bora kuliko zingine zitaungana na wenyeji timu ya taifa ya Gabon kukamilisha timu 16 zitakazoshiriki michuano ya Afcon mwaka 2017 .

No comments:

Post a Comment