Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, April 14, 2015

TAZAMA PICHA 10 ZA HIZI NYUMBA ZENYE MAUMBO YA AJABU

Crocodile-House-Ivory-Coast
Basi mtu wako nikakutana na bonge la HEADLINE mtandaoni yaani.. “10 of the Coolest Homes in the World“, nikaingia faster nijionee PICHA za hizo nyumba kali huko DUNIANI.Nilizokutana nazo kiukweli ilibidi nicheke,alafu nikaona sio vibaya na wewe  uzione labda iko itakayokuvutia na wewe ukatamani siku moja uwe nayo.
Antilia-India
Unaambiwa hii inaitwa Antilia, iko India.
Bio-Climatic-Solar-House-France
Inaitwa Bio Climatic Solar House, iko Ufaransa. Ilivyokaa kaa ni kama siyo mjengo wa kuishi vile.

 
Boeing-727-House-Costa-Rica
Boeing 727 House, hii sio mara ya kwanza kuiona mtu wangu. Haikunishtua nilipoiona tena.
Bubble-House-France
Ilinipa tabu kujua nini kinaendelea hapa. Naona kama mapango mapango tu hivi, lakini ndiyo mjengo huo . Bubble House, iko Ufaransa.
Crazy-House-Vietnam
Duuh, jina lake tu ni balaa . Inaitwa Crazy House, iko Vietnam.
Crocodile-House-Ivory-Coast
Mjengo huu uko Ivory Coast, hivi kama kuna watu mjusi tu wanaogopa, itakuwa kulala kwenye huyu mamba? Nyumba hiyo, inaitwa Crocodile House.
Dar-al-Hajar-Yemen
Hii nayo ni ghorofa ya aina yake . Dar-al-Hajar, iko Yemen.
Shoe-House-South-Africa
Buti la kijeshi??? Hapana, huo ni mjengo kabisa mtu kajitengenezea hapo, inaitwaShoe House, iko South Africa.
The-Toilet-House-South-Korea
Hii ya Korea Kusini nayo iko kwenye list, inaitwa Toilet House, kwa juu ukiicheki ni kama choo kweli.
toilet
Hiyo Toilet House ya Korea inavyoonekana kwa juu.

.
Kama imepinduka hivi.. kumbe hapo ndiyo iko sawa. Hujaipenda hii? Wenyewe wanaiita The Upside Down House, iko Poland.CHANZO MILLARD AYO

No comments:

Post a Comment