Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, April 15, 2015

UEFA CHAMPIONS LEAGUE::ATLETICO WATOKA SARE NA REAL MADRID

2792225200000578-3038873-image-a-38_1429040782992

Cristiano Ronaldo akiruka juu kupiga kichwa mpira
LIGI ya mabingwa barani ulaya imeendelea usiku huu kwa mechi mbili za robo fainali kupigwa.
Uwanja wa Vicent Calderon, Atletico Madrid wametoka suluhu (0-0) dhidi ya mahasimu wao wa jiji, Real Madrid.
Matokeo haya yanawaweka Atletico Madrid kwani watahitaji kufanya kazi ya
Bale (left) storms towards the touchline as Atletico Madrid's Diego Godin keeps close to the Real Madrid star
 ziada katika dimba la  Santiago Bernabeu.Real Madrid walicheza vizuri na kutengeneza nafasi 

 
kadhaa ugenini, lakini wenyeji walikuwa butu safu ya ushambuliaji kitu kilichowafanya wakose ushindi.
Kama Real watacheza kama leo Bernabeu basi watakuwa na nafasi ya kusonga mbele.
Katika dakika 90′ Real Madrid wamepiga mashuti 8 yaliyolenga lango dhidi ya mawili ya Atletico.
Mbali na hivyo vijana wa Carlo Ancelotti walimiliki mpira kwa asilimia 52 dhidi ya 48 za wenyeji.
Kutokana na presha waliyotoa Real, Atletico wamelazimika kufanya madhambi mara 19 dhidi ya 11 ya vijana wa Bernabeu.
Jumatano ijayo, Real Madrid wanahitaji ushindi wa goli 1-0  au 2-1 ili kusonga mbele na kama Atlectico wanahitaji kusonga mbele nao wanahitaji ushindi kama huo au ushindi.
Wakitoka 1-1, Atletico atasonga mbele kwa faida ya goli la ugenini.
Mechi nyingine usiku , Juventus wameshinda goli 1-0 dhidi ya Monaco.
Goli la Monaco limefungwa na Arturo Vidal kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 57.
Juventus wanahitaji suluhu (0-0) ugenini ili kusonga mbele.
UEFA itaendelea tena leo kwa robo fainali mbili kupigwa, FC Porto wanaikaribisha Bayern Munich, wakati Paris Saint Germain wanaikaribisha FC Barcelona.NA SHAFIH DAUDA

No comments:

Post a Comment