Viongozi wa Serikali ya Mkoa wa kusini Pemba wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla na Mkuu wa Wilaya ya Mkaoni Mhe:Hemed Suleiman Abdalla, wakizungumza na mbunge wa jimbo la Mkanyageni Habibu Mnyaa wakati walipokuwa wakivuka kuelekea kisiwa Panza kwa lengo la kuwafariji wananchi waliopatwa na maafa ya nyumba zao kuezuliwa na upepe.
Wananchi mbali mbali wakiangalia nyumba iliyoangua hasa kufuatia upepo mkali uliovuma katika kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani, Usiku wa Kuamkia Aprili 22 mwaka huu
Miongoni mwa nyumba zilizokubwa na maafa kufuatia upepo mkali uliovuma usiku wa kuamia Aprili 22 mwaka huu, huko katika kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani, upepo huo ulizikomba bati zote katika nyumba hiyo
Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, akiwafariji
wananchi waliopatwa na maafa ya nyumba zao kuezuliwa mapaa na upepo
mkali uliovuma kisiwani humo
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla akiangalia nyumba ilikubwa na maafa baada ya upepo mkali kuezua bati zote, huko Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe:Hemed Suleiman Abdalla.
Muembe ukiwa umengolewa na Upepo mkali uliovuma katika kijiji cha kisiwa Panza, ambapo uliweza kumwangukia ngombe ambaye alikuwa amefunga maeneo hayo na ngombe huyo kuchinjwa
Sheha wa Shehia ya Kisiwa Panza Chumu Abdalla Abdalla, akiwaonyesha viongozi wa Serikali ya Mkoa wa kusini Pemba, Miti aina ya Mikoko iliyoharibiwa vikali na upepo huo ulioleta athari kwa wananchi wa kisiwa Panza
Fundi akikaweka sawa bati iliyokubwa na dhoruba ya upepo mkali katika nyumba ya mwananchi huko kisiwa Panza
Jengo la madrasa ambalo ukuta wake umeanguka chini na paa lake kuezuliwa baada ya upepo mkali uliovuma kisiwa Panza na kusababisha maafa kwa wananchi wa kisiwa hicho
Wananchi wa kisiwa Panza waliopata athari ya nyumba zao kuezuliwa mapaa na upepo mkali uliovuma kisiwani huko, wakiwa na huzuni baada ya viongozi wa serikali ya mkoa kusini Pemba kufika kuwapa pole. Kwa hisani ya ZanziNews (Picha na Abdi Suleiman, Pemba)
No comments:
Post a Comment