Morris Sekwao akiwa na Lulu.
Jamaa ambaye inasemekana
ni rafiki wa karibu wa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ aitwaye Morris Sekwao ‘Junior’ inadaiwa amepata msala
‘hevi’ baada ya kutiwa mbaroni nchini Nigeria akituhumiwa kunaswa na
madawa ya kulevya ‘unga’.Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa familia ya
Junior zilidai kuwa, jamaa huyo alipatwa na mkasa huo hivi karibuni
nchini humo ambapo alikuwa akitokea Bongo na mzigo huo.
Morris Sekwao ‘Junior’ akiwa na sanduku la madawa ya kulevya aina ya Ephedrine alilokutwa nalo.
AKAMATWA UWANJA WA NDEGE NA KILO 25
Chanzo hicho kilidai
kwamba Junior alikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Murtala
Muhammed (MMIA) uliopo Ikeja, Lagos nchini Nigeria, akiwa na madawa hayo aina ya Ephedrine yenye uzito wa kilo 25.Ilidaiwa kwamba Junior ambaye ni rafiki wa mastaa mbalimbali Bongo, alidakwa na polisi wa uhamiaji uwanjani hapo baada ya kutilia shaka begi kubwa alilokuwa amelibeba.
Muhammed (MMIA) uliopo Ikeja, Lagos nchini Nigeria, akiwa na madawa hayo aina ya Ephedrine yenye uzito wa kilo 25.Ilidaiwa kwamba Junior ambaye ni rafiki wa mastaa mbalimbali Bongo, alidakwa na polisi wa uhamiaji uwanjani hapo baada ya kutilia shaka begi kubwa alilokuwa amelibeba.
NI BEGI ZIMA
Ilidaiwa kwamba, baada
ya ukaguzi alikutwa na begi zima la unga wenye ujazo huo wa kilo 25
ambao thamani yake haikuwekwa wazi mara moja.
KAMA MASOGANGE
Chanzo hicho kilizidi
kumwaga ‘ubuyu’ kwamba aina ya madawa aliyokamatwa nayo ni kama yale
aliyokamatwa nayo video queen wa Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ nchini
Afrika Kusini ‘Sauzi’ mwaka 2013.
BOSI YULEYULE
Madai mazito yalishushwa
kwamba ‘doni’ aliyembebesha mzigo (aliyemfanya punda) Junior ndiye
yuleyule aliyedaiwa kumbebesha Masogange.Ilisemekana kuwa baada ya
kukamatwa, uchunguzi wa kipolisi unaendelea nchini humo ambapo kwa
sheria za Nigeria, jamaa huyo akikutwa na hatia anaweza kwenda jela
miaka kadhaa.
NDUGU WAHAHA
Uchunguzi wa gazeti hili
umebaini kwamba kukamatwa kwa Junior kumewashtua baadhi ya ndugu, jamaa
na marafiki zake kwa kuwa hawakuwa wanajua kama ndugu yao huyo anafanya
kazi hiyo.
KAMANDA NZOWA AFIKISHIWA TAARIFA
Kamanda wa Kikosi cha
Kupambana Dawa za Kulevya Bongo, Godfrey Nzowa alipoulizwa juu ya
taarifa za kukamatwa kwa kijana huyo alisema hajazipata lakini aliahidi
kufuatilia ili kupata undani wake.
Kamanda wa Kikosi cha Kupambana Dawa za Kulevya Bongo, Godfrey Nzowa.
KUHUSU JUNIOR
Habari zilizo kwenye
makabrasha ya gazeti hili zinaeleza kuwa Junior ni mtoto wa mjini ambaye
mara nyingi hupenda kuambatana na wasanii mbalimbali Bongo ambapo mara
nyingine husafiri nao nje ya nchi bila kujulikana anapiga dili gani.
NDIYE ALIYEMKIMBIZA LULU USIKU WA KIFO CHA KANUMBA?
Ilidaiwa kwamba usiku wa
kuamkia Aprili 7, 2012 ambapo ndiyo siku kilitokea kifo cha aliyekuwa
mwigizaji mkubwa Bongo, marehemu Steven Kanumba, Junior ndiye aliyedaiwa
kumkimbiza Lulu kutoka nyumbani kwa Kanumba na kwenda naye kwenye
Ufukwe wa Coco kabla ya kukamatwa alfajiri yake maeneo ya Bamaga-Mwenge
jijini Dar
No comments:
Post a Comment