Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, April 9, 2015

VIDEO YA POLISI WA KIZUNGU AKIMPIGA KWA RISASI NA KUMUUA MTU MWEUSI YAZUA UTATA



Polisi wa kizungu wa South Carolina nchini Marekani, jana Jumanne alishtakiwa kwa kosa la mauaji, saa chache baada ya maofisa kutazama video ya kushangaza inayomuonesha akimpiga risasi mgongoni na kumuua mwanaume mwenye asili ya Afrika aliyekuwa akikimbia.

Meya wa North Charleston, Keith Summey alitangaza mashtaka hayo kwenye mkutano na waandishi wa 

 
habari ambapo alisema polisi huyo aitwaye Michael Thomas Slager alichukua uamuzi mbaya.
Aliyeuawa anaitwa Walter Lamer Scott mwenye umri wa miaka 50.
Video hiyo iliyosambazwa kwenye vituo vya runinga inamuonesha ofisa hiyo akimmiminia risasi mgongoni mtu huyo wakati akikimbia.
Mtu aliyechukua video hiyo hajulikani.

No comments:

Post a Comment