Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, April 9, 2015

WATU 10 WAFARIKI DUNIA BAADA YA MABASI YA NGORIKA NA RATCO KUGONGANA

Watu 10 wamekufa katika ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mkata katika Kijiji cha Mbweni Wilayani Handeni Mkoani Tanga majira ya saa 5 asubuhi ya leo.
 Polisi mkoani Tanga wamethibitisha tukio hilo na kusema ajali hiyo imehusisha mabasi mawili ya abiria na gari dogo katika barabara ya Dar es Salaam kwenda Tanga na Arusha.




Kwa mujibu wa Jeshi hilo gari dogo ilikuwa likitaka kulipita lori lililokua mbele yake na ndipo ilipogongana uso kwa uso na basi la RATCO lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dar es Salaam.
 Baada ya Basi la RATCO kugonganana na gari dogo, lilipoteza mwelekeo na kugongana tena uso kwa uso na basi la Kampuni ya Ngolika lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda jijini Arusha.
 Kati ya watu 10 waliokufa wanaume ni watano akiwemo Dereva wa gari dogo na Dereva wa basi la Kampuni ya Ngorika pamoja na wanawake watano wakiwemo watoto wawili.


        Mpaka sasa maiti kumi zimeshatolewa huku jitihada zaidi zikiendelea kujua kama bado wapo ambao wamo ndani ya magari hayo yaliyogongana uso kwa uso au laa.
 Picha hizi ni kwa hisani ya Mtandao wa Mabalozi wa Usalama barabarani Tanzania (RSA).






No comments:

Post a Comment