Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) ,Bwa.Sebastian Ndandala akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.
Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (katikati) akiuliza swali kwa Mratibu wa Mradi wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) hayupo pichani.
Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) ,Bwa.Sebastian Ndandala akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.
PROGRAMU ya Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) imetaja changamoto zinazoukabili mradi huo licha ya mafadikio mengi iliyoyapata wakati mradi huo ukiingia awamu ya nne ya utekelezaji wake.
Mratibu wa Mradi huo,Bwa.Sebastian Ndandala ametaja changamoto hizo leo mjini Kibaha alipokuwa akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari pamoja na waendeshaji wa mitandao ya jamii ikiwa ni hatua ya kushirikisha vyombo vya habari juu ya utekelezaji wa mradi huo.
Mratibu huyo alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ugumu wa kuunganisha mifumo mbalimbali ya kifedha inayotumika serikali ili mifumo hiyo iweze kuongea kwa pamoja, ugumu wa kujenga uwezo katika maeneo ya kitaalamu kama E-procurement na ICTs, Uhaba wa ferdha za ndani katika kutekeleza program na changamoto nyingine katika utekelezaji mradi.IMEANDALIWA NA THE HABARI.COM
No comments:
Post a Comment