Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, May 20, 2015

MWAKILISHI JIMBO LA CHAKE CHAKE APELEKEKA HOSPITALI DAWA NA VIFAA TIBA VILIVYOPITA MUDA WA MATUMIZI


MWAKILISHI viti maalumu wanawake CUF wilaya ya Chake Chake, Mhe. Salma Mohamed Ali (kulia) akimkabidhi dawa na vifaa tiba,   Daktari dhamana wa hospitali ya Chake Chake, Dk. Yussufu Hamad Idd vilivyotolewa na mwakilishi wa Jimbo la Chake chake, Mhe. Omar Ali Shehe, Mei 3 mwaka huu, kabla ya baadhi ya vifaa na dawa hizo kugunduilika kupitiwa na muda wake wa matumizi.
BAADHI ya dawa na vifaa tiba zilizotolewa hivi karibuni na Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake, Mhe. Omar Ali Shehe ambazo tayari zimeshapitiwa na muda wake wa matumizi, ambapo uongozi wa hospitali ya Chake chake umezigundua wakati wakitaka kuzitumia.


MFAMASIA mkuu wa hospitali ya Chake Chake Pemba, Dk.  Kassim Zahir akionyesha vipamba vya kusafisa damu baada ya kung’olewa jino, ambavyo navyo ni miongoni mwa vifaa tiba vilivyogundulika kupitiwa na muda wake, ambavyo vilitolewa hivi karibuni na Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake, Mhe. Omar Ali Shehe, pamoja na dawa nyengine.
DAKTARI dhamana wa hospital ya Chake Chake Pemba, Dk.  Yussuf Hamad Idd, akitoa maelezo jinsi watakavyomkabidhi dawa na vifaa tiba Mwakilishi wa Jimbo la Chake chake, Mhe. Omar Ali Shehe ambaye hivi karibuni alikabidhi dawa hizo ambazo zimegundulika kupitwa na muda wake wa matumizi.(Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment