Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, May 25, 2015

SABABU KUBWA YA MHE.MWIGULU NCHEMBA KUJIUZULU..

Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba
Aliyekua Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara,Mwigulu Nchemba amejiuzulu wadhifa huo.Mwigulu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha,ametangaza kujiuzulu nafasu hiyo jana Jioni katika kikao cha Halmashauri Kuu ya ya Taifa ya CCM,Mjini DodomaAkithibiths tukio hilo,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi ,Nape Nnauye amesema,Mwigulu ameamua kujiuzulu nafasi 



ya Unaibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara kutokana na nia yake ya kutaka kuomba kuwania Urais kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi utakaofanyika Octoba Mwaka huu
"Mwigulu alishamwambia nia hiyo Mwenyekiti wa Chama Rais Jakaya Kikwete,nae Rais akamkubalia, na sasa katika kikao ameomba rasmi kujiuzulu na Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete amemkubalia Mbele ya wajumbe wa NEC".amesema Nape
Nape amesema kufuatia uamuzi wa mwigulu kujiuzulu, Mwenyekiti wa Chama Rais Jakaya Kikwete amemteua Msaidizi wake wa maswala ya siasa,Rajabu Ruhavi kuwa Mjumbe wa NEC na Wakati huohuo kamteua kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara Kushika nafasi iliyoachwa na Mwigulu Nchemba

No comments:

Post a Comment