Kikundi cha vijana 40 kiitwacho Wajenzi Isoso Wilayani Kishapu kikiendelea na ufyatuaji matofali ya kufungamana wakati kilipotembelewa na Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya kwa nia ya kuhakiki kazi wanazofanya. Halmashauri ya Wilaya hiyo imewapa vijana maeneo ya kufanyia kazi na mtaji wa kufanyia kazi zao.
Kiongozi wa kikundi cha vijana 40 cha Wajenzi Isoso, Wilayani Kishapu akisoma risala kwa Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya (wa pili kushoto walioketi) mara baada ya Meneja huyo
kumaliza mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kishapu Bi. Jane Mutagurwa ambaye alimhakikishia ushiriki makini wa Halmashauri hiyo katika kuwasaidia vijana kazi, mtaji na maeneo endelevu ya kufanyia kazi yao ya kufytaua matofali yanayofungamana. Aliishukuru NHC kwa msaada wa mashine kwa Halmashauri hiyo ambazo zimewapa vijana ajira.
Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya na Meneja wa NHC Mkoa wa Shinyanga Bw. Ramadhani Macha (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bw. Festo Kang’ombe mara baada ya kufanya mazungumzo naye ya kuhamasisha Halmashauri hiyo kutoa ushirikiano kwa vijana waliopewa msaada wa mashine na NHC ya kuytatulia matofali yanayofungamana.
Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya akiwa katika eneo la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga maarufu kwa ajili ya vijana wa Juakali wanaotengeneza matofali ya kufinyanga na kuchoma, ambapo aliendesha zoezi la kukinyang’anya mashine iliyotolewa na NHC kama msaada kikundi cha vijana cha Amanias katika Manispaa hiyo baada ya kugundua kuwa kikundi hicho kimeacha kutumia mashine hiyo na kujiunga na kazi za juakali za kutengeneza matofali ya udongo wa kufinyanga.
Wakufunzi wa VETA Shinyanga wakiwa eneo la Kata ya Usanda wakimueleza Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya namna wanavyoshiriki kurekebisha hitilafu ndogondogo zinazojitokeza katika mashine za vijana za kufytatua matofali yanayofungamana alipokagua vikundi vya vijana katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Bi. Isabella Chilumba akiueleza ujumbe wa NHC na watendaji wake namna Halmashauri hiyo inavyoshiriki kikamilifu kuwawezesha vijana waliopewa msaada na NHC wa mashine ya kufyatulia. Halmashauri hiyo imewapa vijana mtaji, maeneo ya kufanyia kazi na kazi za kujenga maabara, kuta za shule mbalimbali na majengo mengine ikiwa ni sehemu ya kusaidia kikundi hicho chenye vijana 70 kuwa na ajira endelevu.
Kikundi cha vijana katika Halmashauri ya Ushetu kikijenga ukuta wa shule ya Sekondari Ukune iliyoko kilometa 70 kutoka Kahama kwa kutumia matofali yanayofungamana baada ya kupewa msaada wa mashine za kufyatulia matofali hayo na NHC mwaka 2014.
Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya akiwapa zawadi ya fedha za kuwaongezea hamasa vijana wa kikundi cha vijana wapatao 70 Wilayani Ushetu kama sehemu ya kuunga mkono juhudi zao baada ya kukagua shughuli za maendeleo walizofanya kwa kutumia mashine za kufyatulia matofali yanayofungamana walizopewa na NHC ili kujiajiri.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Bw. Patrick Kalangwa akitoa maelezo ya jinsi kikundi cha vijana waliyopewa msaada wa mashine za kufyatulia matofali na NHC kinavyosaidiwa na Halmashauri hiyo. Hata hivyo, alikiri kuwa shughuli za migodi ya madini zinafanya baadhi ya vijana hao kuacha kutengeneza matofali na kujihusisha na shughuli za uchimbaji wa madini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kahama Mji Bw. Michael Nzengula akitoa maelezo kwa viongozi wa NHC waliomtembelea Ofisini kwake kufahamu namna Halmashauri hiyo inavyoshiriki katika kusaidia vijana wanaotengeneza matofali ya kufungamana kwa kutumia msaada wa mashine walizopewa na NHC.
Meneja wa NHC Mkoa wa Tabora Bw. Erasto France Chilambo akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bw. Florence Mwale ya nia ya NHC ya kuinyang’anya Halmashauri hiyo mashine za kufyatulia matofali walizopewa na NHC baada ya Halmashauri hiyo kutosimamia kikamilifu vijana.
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kaliua Bw. Mabula Isambula akieleza ujumbe wa NHC namna Halmashauri hiyo mpya inavyowawezesha vijana mitaji na maeneo ya kufanyia kazi za kufytaua matofali yanayofungamana kwa kutumia mashine walizopewa na NHC ili kuwezesha vijana kujiajiri.
Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya akizungumza na kikundi cha vijana Wilayani Kaliua waliopewa msaada wa mashine na NHC ili kujiajiri alipowatembelea kuwapa hamasa na kukagua shughuli zao.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Bw. Gervas Magashi aklipokutana na ujumbe wa NHC na kuueleza mkakati wa Halmashauri hiyo wa kusaidia vijana waliyopewa mashine kutengeneza matofali yanayofungamna na NHC ili kujiajiri.
Ofisa Miliki wa NHC Bw. Rockussy Sanka na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC, Bw. Muungano Saguya wakikagua ubora wa matofali yaliyotengenezwa na kikundi cha vijana cha Tujiajiri na Miti ni Mali Wilayani Nzega.
Meneja wa NHC Mkoa wa Singida Bw. Ladislaus Bamanyisa akimpa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Iramba Bi. Halima Mpita hundi kwa ajili ya kusaidia vijana waliyopewa msaada na NHC wa mashine za kufyatulia matofali yanayofungamana
Meneja waHuduma kwa Jamii na Meneja wa Mkoa wa Singida wakiwa katika Halmashauri ya Ikungi kuhakiki shughuli za vijana za kutengeneza matofali yanayofungamana. Vijana hao wameshajenga jengo la Ofisi ya kuendeshea kazi zao.
No comments:
Post a Comment