Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, June 26, 2015

MHARIRI WA MWANAHALISI ONLINE AFARIKI DUNIA

Mhariri  wa Mwana Halisi Online, Edson Kamukara (pichani), amefariki Dunia kwa ajali ya moto nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam jana majira ya saa moja kasorobo jioni, baada ya kulipukiwa na jiko la gesi, habari zilizotufikia sasa hivi zinasema kuwa Polisi wameuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuhifadhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi wa kifo chake.
Ofisa Uhusiano wa NMB, Viccent Mnyanyika akimkabidhi zawadi marehemu Edson Kamukara wakati wa uhai wake kwenye wa utoaji wa tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) zilizofanyika Aprili 24 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment