Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, June 30, 2015

PICHA:::KADO,NIZAR, HABIB KONDO WANUSURIKA KIFO KWENYE AJALI MBAYA YA GARI

Shabani Kado (aliyekaa kwenye tairi) amepata michubuko kidogo kwenye eneo la mkono mara baada ya ajali hiyo
Wachezaji na makocha wa Mwadui FC wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa makiendesha kuelekea Shinyanga kupata ajali na kupinduka mara tano kabla ya kusimama.
Wachezaji walionusurika kwenye ajali hiyo ni golikipa Shabani Kado pamoja na kiungo Nizar Khalfan.
Wachezaji hao wakiwa na makocha Habib Kondo na Khalid ( kocha wa makipa) walikuwa njiani kwenda kujiunga na kambi ya timu yao ya Mwadui FC.

 
“Sababu ya gari kupinduka ilikuwa ni baada ya tairi la nyuma kuchomoka,baada ya hapo gari ilipinduka karibia mara tano,hatukuumia sana isipokuwa mimi tu nilipata michubuko kwenye mkono”,  Shabani Kado ameuambia mtandao huu

No comments:

Post a Comment