Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, June 25, 2015

SPIKA WA BUNGE MHE. MAKINDA AMEAHIRISHA KIKAO CHA BUNGE KUTOKANA NA KIFO CHA MBUNGE WA GEITA MHE DONALD MAX.


Spika wa bunge Mhe.Anna Makinda ameahirisha kikao cha bunge kutokana na kifo cha mbunge wa jimbo la Geita Mhe Donald Kelvin Max kilichotokea katika hospitali ya taifa ya Muhimbili juni 23 mwaka huu.
Akiahirisha kikao cha bunge Mhe.Makinda amesema marehemu amekuwa akiugua kwa muda mrefu hali iliyopelekea kulazwa hospitalini kwa kipindi kirefu ambapo amesema taratibu za mazishi zinafanywa na anatarajiwa kuzikwa jijini Dar es Salaam siku ya jumamosi ya Jun 27.

Aidha wakizungumzia kifo cha marehemu Donald Max, baadhi ya wabunge wamesema marehemu alikuwa ni mcheshi na mwenye kuelewana na wenzake kwa kipindi alichowahi kuhudhuria vikao vya bunge.

No comments:

Post a Comment