KIBANO! Staa wa Bongo Fleva mwenye jina kubwa Afrika, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’, juzikati alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya
‘kutaitiwa’ kwa saa mbili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA) kisa kikiwa wingi wa mabegi (3) makubwa aliyoshuka nayo akitokea nchini
Afrika Kusini ‘Sauzi’, Ijumaa Wikienda linakupa ‘unyunyuz’ kamili.
Staa huyo akingia ndani kufuatilia ama nini kinaendelea
dhidi ya mizigo yake.KUHUSU STAKABADHI
Kuhusu stakabadhi zisizokuwepo, ilibidi Diamond ampigie simu
‘mdogo wake’ (si wa tumbo moja) aliyejulikana kwa jina la Q-Boy ampelekee kwani
alitua nazo Bongo siku moja kabla, yaani Juni 25.
NDANI YA MABEGI
Ndani ya mabegi hayo, kulikutwa kamera, maiki na vifaa vya
studio.
Chanzo chetu kilichokuwa ndani ya jengo la kutokea abiria kililiambia Kilisema, maafisa ukaguzi wa uwanja huo walimtilia shaka Diamond hivyo ikawalazimu wayakague mabegi hayo hadi ndani lakini pia walimkuta ana upungufu wa stakabadhi za mizigo hiyo.
IMANI YA WAPEKUAJI
Shuhuda mmoja ambaye Ijumaa Wikienda lilimkuta nje ya chumba
ambacho Diamond alikuwa
akipekuliwa, alisema maafisa hao waliamini msanii huyo
alikuwa ameshuka na madawa ya kulevya ‘unga’.“Unajua mastaa siku hizi
wanaongoza kwa kubeba unga. Sasa serikali iko makini nao sana. Ndiyo maana
wengi wao wakipita hapa wanakaguliwa kuliko abiria wengine,” alisema mtu huyo
aliyejitambulisha kuwa ni dereva wa teksi uwanjani hapo.
DIAMOND APIGWA PICHA, AONGEA NA WIKIENDA
Paparazi wetu aliendelea kuganda mlangoni hapo hadi Diamond
alipotoka na kumfotoa picha mbalimbali na baadaye alimfuata hadi kwenye gari
aina ya Toyota Lexus na kumuuliza kama anajua kisa cha kupekuliwa kwa muda
mrefu vile.
“Nilikuwa na mizigo naishughulikia ili itoke hivyo kuna
mambo pia tulikuwa tunapishanapishana pale maana walihitaji nilipie ushuru
wakati vifaa vya studio tulishaambiwa ni ‘free’ (bure). Pia kulikuwa na risiti
za mizigo ambazo zilikuwa hazionekani, kumbe Q-Boy alitangulia nazo jana mimi
nikawa nimesahau.
“Ila wao walikuwa wakijiridhisha kwenye mizigo yangu.
Walifikiri nimebeba unga,” alisema Diamond.
HALI YA SASA UWANJANI
Mbali na Diamond kupekuliwa kwa muda mrefu, kwa sasa abiria
wanaoingia na kutoka kwenye uwanja huo wamekuwa wakikaguliwa kwa umakini ili
kubaini uhalali wa mizigo yao lengo kubwa ni kudhibiti uingiaji au utokaji wa
madawa ya kulevya ambapo serikali imeweka umakini katika kupambana na biashara
hiyo haramu.
CHRISTIAN BELLA
Ukiachana na Diamond, mastaa wengine waliowahi kukumbana na
pekuapekua kama hiyo ni Mkurugenzi wa Bendi ya Malaika, Christian Bella na
mtangazaji wa Radio Time FM, Hadija Shaibu ‘Dida’.
Bella yeye alikumbwa na adha hiyo, mwaka juzi, usiku wa saa
nane akiwa anatokea nchini Uturuki na Ndege ya Shirika la Turkish Airways.
Dida naye ilikuwa mwaka 2012 ambapo alikumbwa na pekuapekua
hiyo alipoingia uwanjani hapo kuelekea nchini Thailand kwa shughuli za
kibiashara.
No comments:
Post a Comment