Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, June 5, 2015

UCHAGUZI WA RAIS NA WABUNGE BURUNDI WAAHIRISHWA


SERIKALI ya Burundi imetangaza kuwa uchaguzi wa Rais na Wabunge uliotarajiwa kufanyika mwezi huu umeahirishwa mpaka tarehe nyingine zitakazotangazwa.
Vurugu Burundi.

Msemaji wa Rais Nkurunziza, Wily Nyamitwe amesema kuwa tarehe hizo zitapangwa na wasimamizi wa uchaguzi wa nchi hiyo hivi karibuni.


Mabadiliko hayo yamekuja kutokana na taifa hilo kuingia kwenye machafuko tangu Rais Piere Nkurunziza kutangaza nia ya kuongoza kwa awamu ya tatu.

Umoja wa Mataifa umeelezea jinsi mgogoro huo ulivyoongeza idadi ya wakimbizi wanaoikimbia Burundi, hivyo kumtaka rais huyo kuachia ngazi mwezi huu kama makubaliano ya Azimio la Arusha yalivyoelekeza.

Uchaguzi wa wabunge ulitarajiwa kufanyika kesho Ijumaa (Juni 5) na wa urais ulipangwa Juni 26, mwaka huu.

Habari kwa hisani ya BBC.

No comments:

Post a Comment