Timu ya Taifa ya Argentina imetinga kwa kishindo hatua ya fainali ya Copa America baada ya kuitandika Paraguay kipigo cha mbwa mwizi cha magoi 6-1 katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa usiku wa kuamkia leo.
Mabao ya Argentina yamefungwa na Marcos Rojo (15), Javier Pastore (27), Angel Di Maria (47, 53), Sergio Aguero (80) na Gonzalo Higuain (83), huku goli la kufutia machozi kwa Paraguay likifungwa na Lucas Barrios (43).
No comments:
Post a Comment