Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, July 13, 2015

AZAM YAIPIGA COASTAL 1-0 MKWAKWANI

Kikosi cha Azam FC ‘Wanalambalamba’ kimeendeleza ushindi kwenye ziara yake mkoani Tanga baada ya hii leo baada ya kuibuka kidedea kwa kuigaragaza Coasta Union ‘Wagosi wa Kaya’ kwa goli 1-0 goli lililofungwa na Ame Ally ‘Zungu’ kwenye mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kuelekea kwenye mashindano ya Kagame Cup pamoja na ligi kuu Tanzania bara kwa msimu ujao.

 
Jana Azam walicheza na African Sports ya Tanga na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 goli lililofungwa na mshambuliaji John Bocco ‘Adebayor’.

No comments:

Post a Comment