Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, July 29, 2015

CECAFA:Gor Mahia yafuzu nusu fainali

Mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Kenya, Gor Mahia wameendeleza fomu yao bora katika kombe la CECAFA kwa kuilaza Malakia ya Sudan Kusini kwa magoli mawili kwa moja na kufuzu kwa nusu fainali.
Beki wa Uganda, Godfrey Walusimbi ALIGEUKA KUWA MFUNGAJI NA KUTIA WAVUNI MAGOLI MAWILI.
Mfungaji matata, Michael Olunga anayesakwa kutokana na ufungaji wake, alimuandalia pasi Walusimbi katika dakika ya 3 naye walusimbi hakuchelea kuipa Gor uongozi.

Gor ilizidisha uongozi wake kupitia Walusimbi KATIKA dakika ya 28 na kuwafanya mashabiki wa Gor waliokuwa katika uwanja wa kitaifa wa Dar Es Salaam.
Kipa Boniface Oluoch ambaye amekuwa na fomu nzuri ya kutofungwa kwa zaidi ya mechi kumi kwenye ligi KUU NCHINI Kenya alifanya vyema langoni kwa kuzaba shuti ya David Dada kunako dakika ya 13
Kipindi cha kwanza kilikamilika Gor ikiongoza kwa magoli mawili kabla ya Thomas Jacob kuipa Malakia matumaini kwa kuelekeza mpira uliorushwa na Wisely Arasa's langoni katika dakika 66.
Mkufunzi wa Al Malakia, Ramzi Sebit amelaumu usimamizi wa mechi kwa kupoteza.
''Mwamuzi hakufaya usimamizi bora wa mechi'' alidai.
Mpinzani wake, Frank Nuttal, anayeifunza Gor Mahia, amefurahia ushindi huo huku akiongeza kuwa wanalenga kufanya vyema katika nusu fainali.
Gor, iliyoaga Makala ya kombe hilo mwaka uliopita sasa itamenyana na Al Khartoum ya Sudan.
Al Khartoum, iliyochukua nafasi ya El Merreikh kuwakilisha Sudan kwenye kombe hilo, iliicharaza APR ya Rwanda kwa magoli manne bila jibu.bbc swahili

No comments:

Post a Comment