Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva akibadilishana mkataba na kocha mpya wa mazoezi ya viungo Dušan Momčilović.
Kocha huyo kutoka Nchini Serbia ana uzoefu mkubwa katika fani ya
mpira wa miguu hususani mazoezi ya viungo. Kocha Dušan amefundisha klabu
mbalimbali duniani kwenye Nchi kama Malaysia, Indonesia, Georgia ambako
Alikuwa kocha wa mazoezi ya viungo wa klabu ya FC DINAMO ambayo
ilicheza mechi za awali ya klabu bingwa ya Ulaya-UEFA, Bosnia and
Herzegovina, Oman na Belgrade
Kocha Dušan pia ana uzoefu wa kufundisha na kufanya kazi Afrika,
ameshawahi kufanya kazi na
kufundisha timu ya FC SOGOR –Tobruk – Libya.
kufundisha timu ya FC SOGOR –Tobruk – Libya.
Kocha Dušan ni muhitimu wa Digrii ya Mazoezi ya Viungo jijini
Belgrade akiwa amejikita Zaidi kwenye mazoezi ya viungo na kujenga
mwili.
Klabu ya Simba inafuraha kubwa kuingia mkataba na kocha Dušan
Momčilović mwenye uzoefu na weledi wa kutosha, tunaamini atakuwa chachu
ya mafanikio pia kunoa vipaji vya wachezaji wa Simba.
No comments:
Post a Comment