Waamuzi wa mchezo kati ya timu ya taifa ya ska ya Tanzania chini ya mkiaka 20 ya The Tanzanite wakiingia uwanjani wakati timu hiyo ilipopambana na Zambia katika mchezo wa kufuvu kucheza fainali ya Kombe la Dunia kwa Wanawake.
Kikundi cha ushangiliaji kikishangilia timu ya The Tanzaniate.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania, ‘The
Tanzanite’ Shelder Boniface akichuana na
mchezaji wa timu ya Zambia, Esther Mukwasa katika mchezo wa kutafuta tiketi ya
kufuzu fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya miaka 20, uliofanyika
kwenye Uwanja wa Chamazi jijini la Dar es Salaam jana. Zambia
ilkishindi 4-0.
Ireen Lungu akimiliki mpira.
Golikipa wa timu ya Zambia, Hazel Natasha akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
Benchi la ufundi la timu ya taifa ya Tanzania, ‘The Tanzanite’
chini ya kocha wake, Rogasian Kaijage
(kushoto) akifuatilia mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la
Dunia kwa Wanawake chini ya miaka 20 dhidi ya Zambia uliofanyika kwenye Uwanja
wa Chamazi Dar es Salaam. Zambia ilkishindi 4-0.
Baadhi ya wachezaji wa The Tanzanite wakilia baada ya kupoteza mchezo kwa kipigo cha 4-0.
Wachezaji wa timu ya Tanzania 'The Tanzanite' mara baada ya mchezo kumalizika.
Waamuzi wakitoka baada ya mchezo kumalizika.
No comments:
Post a Comment