Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, August 28, 2015

DKT MAGUFULI: UKINUNUA MADARAKA IPO SIKU UTAWAUZA ULIOWANUNUA

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji wa Mbalizi  mkoa mpya wa  Songwe,katika mkutano wake wa kampeni uliohudhuriwa maelfu ya wananchi, Dr. John Pombe Magufuli amewaomba wananchi wa Mbalizi kummpa kura za ndiyo ili aweze kuongoza watanzania na kutatua matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii ya watanzania wa hali ya chini.


 
Amesema ametumikia nchi hii kwa miaka 20 serikalini akiwa Waziri na amekuwa mkweli na muwazi ndiyo maana ameweza kuisimamia vizuri kila wizara au jukumu alilopewa na wakubwa wake akiwatumikia Watanzania na sasa anaomba nafasi ya urais ili aweze kutekeleza vyema jukumu lake la kuwatumikia Watanzania .

Aliongeza kuwa ndiyo maana katika mchakato mzima wa kugombea urais ndani ya Chama cha Mapinduzi  alifanya kimya kimya na hakutumia fedha yoyote hivyo hakuna mtanzania yeyote anayemdai fedha ila anadaiwa utumishi uliotukuka wenye uaminifu, kujituma na kutetea maslahi ya watanzania na taifa kwa ujumla katika  taifa la Tanzania, Ameongeza kwamba ukitumia fedha kuingia madarakani na kununua madaraka ipo siku utawauza uliowanunua.


Wananchi waliokusanyika kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika stendi ya mabasi mjini Mbalizi wakishangilia huku wakipiga makelele kwamba anatosha na anafaa kuwa Rais na wameahidi kumpigia kura ya ndiyo.
Wafuasi wa chama cha CCM na wananchi wakiwa wamekusanyika katika stendi ya mabasi mjini Mbalizi wakimsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ambapo aliwahutubia na kuwaomba wampe kura ya ndiyo ili aweze kuwoangoza katika awamu ya tano.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufulia akisisitiza jambo wakati akiwahutubia wakazi wa Mbalizi na kuendelea kusisitiza kuwa elimu itakuwa bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne,kuongeza maslahi ya walimu pamoja na jeshi la polisi.
Wakazi wa mbalizi wakimsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akimwaga sera za kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kituo cha mabasi Mbalizi.
Maelfu ya watu wakiwa na kiu kubwa ya kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha CCM mjini Mbalizi.

Wananchi wa mji wa Chunya mjini wakishangilia ujio wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli katika viwanja vya Saba Saba Chunya mjini kwenye mkutano wa kampeni,ambapo Magufuli aliwahutubia wananchi hao na kuwaomba kura ya ridhaa ya kuwaongoza kwa kipindi kijacho cha awamu ya tano.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli,alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Makongorosi kuwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni.
Wananchi wa Makongorosi wakimsikiliza kwa makini  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mjini hapo kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi wa Makongorosi wakimshangilia Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mjini hapo kwenye mkutano wa kampeni.

PICHA NA MICHUZI JR-CHUNYA


No comments:

Post a Comment