Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, August 27, 2015

MGODI WA BUZWAGI WAZINDUA LIGI YA MAHUSIANO-KAHAMA.

Baadhi ya Maafisa kutoka Mgodi wa Buzwagi wakifatilia mashindano hayo wakati wa ufunguzi, kutoka kushoto ni Bwana, Jamal Rwambol, (Security Operations Section Leader), George Mkanza-(Sustainability Manager), Amos John – (Commercial Manager and Acting Mine General Manager), Bahati Mwambene-Community relations section Leader na Magesa Magesa-(Stakeholder engagement & communications officer)
Bwana Jamal Rwambol Security Operations Section Leader wa mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo.

Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Amos John  akizungumza wakati  wa uzinduzi wa mashindano hayo.
Mgeni Rasmi Kaimu Meneja wa Mgodi wa Buzwagi akikagua timu ya Star boys wakati wa mechi ya ufunguzi.
Baadhi ya timu zinazoshiriki katika mashindano hayo zikiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufunzi wa ligi hiyo.
Kikosi cha Timu ya Majimaji kutoka kata ya Mwendakulima.
Kikosi cha Timu ya Star Boys.
Baadhi ya timu zinazoshiriki mashindano hayo kwa uoane wampira wa miguu na Soka. 
Bwana Amos John Kaimu meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi akifunga goli kuashiria kufungua michezo hiyo.
Moja kati ya hekaheka wakati wa mechi ya ufunguzi ambapo timu ya majimaji yenye jezi ya njano iliibuka kidedea dhidi ya Star boys baada ya kuitandika bila huruma goli tatu kwa moja (3-1)


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliyekuwa mkoani Shinyanga.

Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kupitia idara yake ya mahusiano ya Jamii imezindua mashindano ya mpira wa miguu na ule wa pete, kwa timu kutoka kata ya Mwendakulima wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Ligi hiyo ambayo imepewa jina la Mahusiano Cup, ikiwa na ujumbe wa Kuhamasisha masuala ya Usalama, Mahusiano na Maendeleo baina ya wenyeji na mgodi wa Buzwagi itahusisha timu tisa za mpira wa miguu na timu nane za mpira wa pete, ambapo kupitia ligi hiyo itaundwa timu moja ya kata ambayo itakuwa ikishiriki ligi za wilaya.
Akizindua ligi hiyo Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Amos John amesema, kupitia mashindano hayo ambayo yamelenga kujenga mahusiano baina ya Mgodi na wenyeji kwa kuimarisha usalama na kuhamasisha shughuli za maendeleo miongoni mwa jamii.
Aidha kaimu meneja huyo amewaasa vijana hao kuonyesha uwezo mkubwa wakati wote wa mashindano kwani kupitia michezo hiyo baadhi ya vijana watakaofanya vizuri watachaguliwa kuunda timu ya kata hiyo ambayo itakuwa ikishiriki michezo mbalimbali kwa ngazi ya wilaya.
Awali Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Bwana  Julius Masubo Kambarage  ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo imekuwa ikifanya katika kuhamasisha na kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo michezo.
“Sisi kwetu kupata mashindano kama haya ni fursa ya pekee sana katika kuhakikisha shughuli za michezo katika halmashauri yetu zinatekelezwa. Tutakacho kifanya kwa sasa ni kuhamasisha hizi timu zisajiliwe ili baadae ziweze kushiriki mashindano makubwa kwa sababu miongoni mwa hawa vijana wapo wenye vipaji vikubwa ila ni fursa tu hawajapata” Alisema Kambarage.
Kwa Upande wake Mratibu wa Mashindano hayo ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Buzwagi Bwana Bahati Mwambene amezitaja timu zinazoshiriki mashindano hayo kuwa ni Tembo,Star Boys,Shehena, zote kutoka mtaa wa Chapulwa. Timu nyingine amezitaja kuwa ni Majimaji, Unity, Budushi, za mtaa wa Mwendakulima, na nyingine ni Israel, Busalala na Miembeni zote hizi ni kutoka mitaa ya Busalala na Mwime.
Aidha Bwana Mwambene amesema kabla ya Kuanza kwa mashindano hayo timu zote zimekabidhiwa vifaa mbalimbali vya michezo kama vile seti za jezi kwa timu zote pamoja na mipira, ambavyo amesema pamoja na zawadi za washindi vimegharimu zaidi ya shilingi za kitanzania milioni ishirini na mbili na laki sita.
Ligi hiyo ambayo inafanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mwendakulima imeanza tarehe 23 mwezi wa nane na inatarajiwa kumalizika tarehe 05 mwezi wa tisa ambapo mshindi wa kwanza kwa kila mchezo atajinyakulia kikombe pamoja na pesa taslimu laki tatu, huku mshindi wa pili akiondoka na laki mbili na nusu na mshindi wa tatu akiondoka na shilingi laki mbili.


No comments:

Post a Comment