Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, August 27, 2015

MOTO WATEKETEZA MAROLI MAWILI YA MAFUTA MWANZA


Malori mawili ya mafuta yameteketea kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya Jenereta iliyokuwa inatumika kushusha mafuta kutoka ndani ya malori hayo kwa ajili ya kuyahifadhi kwenye kisima cha mafuta cha sasa kazi kilichopo eneo la Butimba kona jijini Mwanza na kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi,sambamba na kuteketea kwa pikipiki moja mali ya Ayoub Ismail.
Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea majira ya saa 4.30 asubuhi wanasema malori hayo aina ya SCANIA – moja lenye namba za usajili T 509 AFD na Tela 

 
lake namba T 592 ACL lililokuwa limebeba lita 35 za mafuta ya Dizeli pamoja na lori jingine lenye namba za usajili T 674 AHH ambalo lilikuwa limeegeshwa kando kidogo ya kituo hicho cha mafuta cha sasa ni kazi yameteketea na kusababisha wingu kubwa la moshi mweusi,huku juhudi za wananchi kuzima moto huo uliokuwa ukiwaka kwa kasi ya ajabu zikigonga mwamba.
Muda mfupi magari ya jeshi la zimamoto na uokoaji jijini Mwanza yakawasili katika eneo la tukio yakiwa yamesheheni askari na kazi ya kuzima moto huo ikaanza rasmi,huku baadhi ya wananchi waliofika mapema kushuhudia tukio hilo wakieleza chanzo kilichosababisha malori hayo kushika moto na kuteketea. 

No comments:

Post a Comment