Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, August 13, 2015

TANGAZO MUHIMU KWA UMMA JUU YA KUIBIWA KWA STAKABADHI ZA SERIKALI (EXCHEQUER RECEIPT VOUCHERS)




Ofisi ya Madini, Kanda ya Mashariki Dar es Salaam inautangazia Umma kwamba, usiku wa Jumapili ya kuamkia tarehe 03-08-2015 wezi walivunja Ofisi ya Madini Kanda ya Mashariki iliyopo Upanga, Dar es Salaam na kuiba vitu mbalimbali vya Ofisi vikiwemo vitabu vya Stakabadhi za malipo ya Serikali.
Katika tukio hilo, stakabadhi namba ERV 6361601-6361800, na ERV 6361201, 6361202, 6361203, 6361204 ziliibwa.
Aidha, vitabu vipya vinane (8) vyenye Stakabadhi namba 6360201-6360400, 6360401-6360600, 6360601-6360800, 6360801-6361000, 6361001-6361200, 6361205-6361400, 6361401-6361600 na 6361801-6362000 viliibwa, kuharibiwa na kutupwa nje ya ofisi ya madini.

 
Kwa taarifa hii, tunautangazia Umma kwamba stakabadhi zote zilizoibwa na kuharibiwa hazitumiki na malipo yote yatakayofanyika kupitia stakabadhi tajwa hapo juu yatakuwa ni batili.
Tunaomba yeyote mwenye taarifa sahihi zitakazoweza kusaidia kukamatwa kwa wezi husika kutoa taarifa katika Ofisi ya Madini au kituo chochote cha Polisi kilichopo karibu.

Imetolewa na:
Kamishna Msaidizi wa Madini

Kanda ya Mashariki – Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment