Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, September 1, 2015

GARY NEVILLE ATUPA DONGO KWA VAN GAAL BAADA YA KIPIGO CHA SWANSEA

Wakali watatu wa Manchester United Wayne Rooney, Memphis Depay na Daley Blind wakionekana wenye nyuso za huzuni baada ya kipigo cha jana kutoka kwa SwanseaGary Neville amesema kwamba, Man Unted inahitaji kipa mpya, beki na mshambuliaji mpya baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Swansea jana.
Van Gaal alitoa madai ya wazi kuwa United ‘walitawala mchezo kwa takribani dakika 85 ’ za mchezo, ambapo walijipatia bao lao kupitia kwa Juan Mata kabla ya Andre Ayew na Bafetimbi Gomis kupeleka kilio kwa wakali hao wa Old Trafford.Sergio Romero, kwa mara nyingine tena alianza mbele ya David de Gea ambaye mpaka sasa mustakabli wake bado haupo wazi, huku Muargentina huyo akifungwa goli la kizembe na Gomiz ambaye alifunga goli la ushindi kwa Swansea. Hivyo basi, Neville ameelekeza lawama zake kwa washambuliaji wa timu hiyo kwa kukosa makali pindi wawapo langoni. 
Makosa ya kipa wa Man U, Sergio Romero yaliigharimu United kufungwa hapo jana.
 Gary Neville.

 
Mshambuliaji wa Swansea Bafetimbi Gomis akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Manchester United jana. 
Neville alisema: ‘ Wanatakiwa kumalizana na suala la kipa. Hilo ni tatizo kubwa sana. Manchester United inahitaji mshambuliaji mpya, wambakishe de Gea na sasa tayari John Evans ameshaondoka, hivyo na beki wa kati pia anahitajika.’

No comments:

Post a Comment