Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, October 24, 2015

DAWA ZA KULEVYA HEROINE NA COCAINE ZATEKETEZWA CHINI YA UANGALIZI MKALI JIJINI DAR

Sehemu ya Dawa za kulevya zilizoteketezwa jana katika Kiwanda Cha Saruji Cha Wazo Hill Jijini  Dar es Salaam uku zikisimamiwa na majaji wa mahakama Kuu, jeshi la Polisi pamoja na mamlaka ya kudhibiti Dawa za kulevya hapa nchini
 Sehemu ya Kinu cha Kiwanda Cha Saruji Cha Wazo Hill Jijini  Dar es Salaam  ambako dawa za kulevya zimeteketezwa jana chini ya uangalizi mkali . Akizungumza  na waandishi wa habari mara baada ya kuzichoma moto katika kinu hicho Jaji  wa Mahakama Kuu Edison Mkasimongwa alizitaja aina ya dawa hizo kuwa  ni Heroine mifiko 179 na Cocaine mifuko 81 zenye thamani ya Shilingi Bilioni tano ambapo  zilikuwa na Gram 175,000 ambazo zilikamatwa miaka kadhaa Mbezi Jogoo jijini Dar.
Jaji wa Mahakama Kuu Edison Mkasimongwa(kulia) akihakiki sehemu ya kinu cha kuchomea madawa hayo ya kulevya uku akisindikizwa na Mkurugenzi wa Mashtaka  Biswalo Mganga(kushoto) katika Kiwanda Cha Saruji Cha Wazo Hill Jijini  Dar es Salaam

 
Hii ndio sehemu ya mfuniko wa kinu kilichotumika kuchomea dawa za kulevya
Majaji kutoka mahakama kuu pamoja na polisi wakifuatilia kwa umakini uteketezaji wa dawa za kulevya
Askari wakifungua maboksi yaliyokuwa yamebeba dawa hizo za kulevya kwa ajili ya kuziteketeza katika kinu cha kiwanda cha Saruji hapa jijini Dar.
Jaji wa Mahakama Kuu Edson Masimongwa(kushoto) akifungua moja ya boksi lililobeba dawa za kulevya kwa ajili ya kuhakiki pamoja na kuziteketeza dawa hizo
Askari akizihakiki dawa za kulevya kwa kuzihesabu ili kuziteketeza ambapo zoezi hili lilifanyika katika Kiwanda Cha Saruji Cha Wazo Hill Jijini  Dar es Salaam jana mchana
Mfanyakazi kutoka kapuni tya Saruji ya Twiga akiziteketeza dawa uku akisimamiwa na jeshi lapolisi, maofisa wa mahakama pamoja na viongozi wa kudhibiti Dawa za kulevya hapa nchini hapo jana katika kiwanda hicho
Maofisa kutika mahakama pamoja na maofisa kutika mamlaka ya udhibiti wa dawa za kulevya wakifuatilia tukio la kuteketeza dawa hizo

No comments:

Post a Comment