MKURUGENZI
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI), Dk.
Mwele Malecela akifungua mkutano huo wa pili wa mwaka wa kimataifa wa wataalam
wa kudhibiti Mbumbu kwa Nchi zisizofungamana Afrika (PAMCA) jijini
Dar es Salaam.
Washiriki
wa mkutano huo umeshirikisha Wanasayansi watafiti kutoka nchi mbalimbali za
Afrika. Mkutano
wa kwanza wa Kimataifa wa PAMCA ulifanyika jijini Nairobi Kenya 2014.
Dk
Malecela amesema kuwa mkutano huu unakutanisha wataalam wa kupambana na Mbu
Afrika nzima wataweza kukaa na kubadilishana uzoefu wao juu ya njia za
kupambana na mbu.
“Wataalam
hawa wanakutana kupitia umoja wao wa PAMCA utawawezesha wataalam hawa
kujadiliana njia mbalimbali za kuweza kupambana na mbu hasa kutokana na tabia
za mbu za kubadilika badilika na kufanya kuwa sugu kwa madawa mbalimbali,”alisema
Dk Malecela.
Amesema
wataalm wa Mbu wanapokutana katika mikutano kama hii huwawezesha wataalam
kupata ujuzi mpya wa kuweza kupambana na kukabiliana na mbu.
Mbu
huambukiza magonjwa mengi, hivyo kuwa na taasisi ya wataalm wa Waafrika wenyewe
ni jambo la kujivunia sana hivyo mkutano huu utaweza kufanikisha kupata vitu
mbalimbali kutokana na mada zitakazo wasilishwa na ambazo zitaingizwa katika
mipango na sera mbalimbali katika nchi zetu.
Mapema
akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kimadawa Kenya (KEMRI), Musau Kyanesa amesema
lengo la kuanzishwa kwa PAMCA ni kutafuta njia stahiki ya kupambambana na mdudu
mbu ambae hueneza magonjwa mbalimbali ambayo huathiri binadamu.
“Itakuwa
ni jambo jema sana kama tutaweza kumdhibiti mdudu huyu mbu ambaye anaeneza
magonjwa haya na kufanikiwa kwa hilo tutaweza kuendeleza afya za wananchi wetu
kwa nchi za Afrika, maana Afrika ndio tunapata shida sana na mdudu huyu mbu,”
alisema Kyanesa.
Aidha Kyanesa ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa KEMRI amesema wameandaa mpango wa kuhamasisha wanafunzi vyuoni kujikita katika sayansi ya Mbu ili kupata watalaam wengi wakuweza kukabiliana mbu Kenya na Afrika kwa ujumla.
"Tunaandaa mpango wa kuhamasisha vijana kusomea na hatimaye kuwa na utaalm juu ya mapambano na kufanya tafiti za mbu, kwa kugharamia masomo yao kutokana na upungufu wa wataalam kulingana na tatizo lenyewe,"alisema Kyanesa.
Mwenyekiti wa Bodi ya PAMCA, Prof Charles Mbogo akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo.
Washiriki wakisikiliza mada mbalimbali katika siku ya kwanza ya mkutano huo, Dar es Salaam leo.
Rais wa PAMCA tawi la Tanzania, Dk Stephen Magesa akizungumza katika mkutano huo.
Mkuu wa NIMRI Tanzania, Dk.
Mwele Malecela akizungumza na Mkurugenzi Msaidizi wa KEMRI kutoka Kenya, Musau Kyanesa baada ya ufunguzi wa mkutano huo.
Prof Wen Kilama akiwasilisha mada juu ya Maadili ya Utafiti wa Afya hususani Maleria Afrika .
Prof Wen Kilama akiendelea na uwasilishaji wa mada yake. Prof Kilama ni Mkurugenzi Mstaafu wa NIMR.
Dk Mwele Malecela na washiriki wengine wakifuatilia mada ya Prf Kilama.
Washiriki wakifuatilia mada hiyo.
Picha ya pamoja ya washiriki mkutano huo wakiwa na mgeni rasmi.
No comments:
Post a Comment