Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, October 13, 2015

UBADHIRIFU KIKWAZO CHA USHIRIKA KUSHAMIRI‏

IMG_6069
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida na Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon Manyama wakipitia makabrasha ya mafunzo ya siku moja juu ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika (SACCOS na VICOBA) na Maafisa Ushirika wa kutoka Wilaya za Bunda, Bukoba na Sengerema yaliyoandaliwa na ESRF na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo (UNDP) kabla ya kuwasili mgeni rasmi kufungua mafunzo hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza.
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
IMEELEZWA kuwa matatizo ya uendeshaji wa vyama vya ushirika hasa ya kutokuzingatiwa kwa sheria na kanuni za ushirika, wizi na ubadhirifu wa mali yamedhoofisha sana ushirika Mkoani Mwanza.
Hayo yamesema na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Manju Msambya kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo, Mwanza.
 
Alisema kutokana na ukweli huo ni vyema vyama vya ushirika vikawa makini katika uchaguzi na kuhakikisha kwamba kila wanapofanya uchaguzi wanachagua viongozi wazuri wenye uchungu na maendeleo ya ushirika na siyo wanaotanguliza maslahi yao binafsi na kupuuza ya wengi.
“Tusaidiane kupambana na maovu na kujenga ushirika ulio imara.” Alisema.
Alisema pamoja na changamoto za kiuongozi Mwanza kwa sasa imepiga hatua kubwa upande wa SACCOS na VICOBA.
IMG_6261
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida akifurahi jambo na Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya Ilemela, Manju Msambya aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kufungua mafunzo hayo mara tu baada ya kuwasili ukumbini hapo.
“... hatuna budi kuyalinda mafanikio haya kwa uwezo wetu wote. Mafanikio hayo tutayalinda kwa kuhakikisha kuwa SACCOS zinaendeshwa kitaalamu na kwamba sheria na kanuni za ushirika zinazingatiwa ipasavyo.” alisema
Aidha Mkuu huyo wa mkoa, alishukuru ESRF na UNDP kwa kusaidia kugharamia mafunzo kwa watendaji wa SACCOS ili waweze kufanyakazi zao kwa misingi stahiki.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida alisema lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha ushirika wa akiba na mikopo mkoani Mwanza.
Akizungumzia historia ya mradi alisema wao kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) pamoja Tume ya mipango, walianza kutekeleza mradi wa kukuza uchumi, kuleta maendeleo endelevu kupitia utunzaji mazingira, usawa wa kijinsia na kupunguza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yaani (PEI) toka mwaka 2014.
IMG_6398
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida akitoa maelezo ya utangulizi juu ta madhumuni ya mafunzo hayo kwa washiriki kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi.
Alisema tafiti mbili chini ya mradi wa PEI zilizofanyika katika wilaya za Bunda, Ileje, Sengerema, Bukoba vijijini, Ikungi na Nyasa kubaini changamoto na fursa zinazopatikana katika wilaya hizo.
Alisema matokeo ya tafiti yalionyesha umuhimu wa kuzipa uwezo taasisi za kifedha kama SACCOSS, VICOBA na vikundi mbalimbali vya kifedha kwa kuzijengea uwezo wa kitaaluma na kifedha.
Alisema hata hivyo pamoja na matokeo hayo Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) lilitenga na kutoa fungu la fedha na kuipatia benki ya Twiga ili kukopesha kwa riba nafuu kwenye taasisi kama SACCOSS na VICOBA kwa lengo kuu kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi ili waweze kupata fursa ya kukuza mitaji yao na kuwafanya waweze kutekeleza fursa hizi katika maeneo yao.
Wataalamu mbalimbali wakiwemo Dk. Jones Kaleshu kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi walishiriki kutoa mada.
IMG_6488
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya Ilemela, Manju Msambya akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku moja juu ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika (SACCOS na VICOBA) na Maafisa Ushirika wa kutoka Wilaya za Bunda, Bukoba na Sengerema yaliyoandaliwa na ESRF na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo (UNDP) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza.
IMG_6482
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya Ilemela, Manju Msambya akisisitiza jambo kwa washiriki (hawapo pichani).
IMG_6182
Pichani juu na chini ni baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Ushirika (SACCOS na VICOBA) na Maafisa Ushirika wa kutoka Wilaya za Bunda, Bukoba na Sengerema wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani).
IMG_6173
IMG_6426
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon Manyama akitoa maelezo kuhusu mradi wa PEI na salamu kutoka UNDP kwa washiriki wa mafunzo hayo.
IMG_6162
Mkuu wa Idara ya Maarifa na Mawasiliano wa ESRF ambaye pia ni Mratibu wa mradi wa Kukuza Uchumi, Kuleta Maendeleo Endelevu Kupitia Utunzaji Mazingira, Usawa wa Kijinsia na Kupunguza Mabadiliko ya Tabia Nchi, Margareth Nzuki akitowasilisha matokeo ya Tafiti PEI 2014; Mchango wa Huduma za Kifedha (Akiba na Mikopo) katika maendeleo ya jamii vijijini.
IMG_6462
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya Ilemela, Manju Msambya akinyanyua juu kitabu cha "Mwongozo wa Mafunzo ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo, Elimu ya Ujasiriamali na Stadi za Biashara" kama ishara ya uzinduzi rasmi wa mwongozo huo ulioandaliwa na ESRF. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon Manyama (kulia).
IMG_6475
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya Ilemela, Manju Msambya ( wa pili kushoto) aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto), Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon Manyama (wa pili kulia) na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Mawasiliano wa ESRF ambaye pia ni Mratibu wa mradi wa Kukuza Uchumi, Kuleta Maendeleo Endelevu Kupitia Utunzaji Mazingira, Usawa wa Kijinsia na Kupunguza Mabadiliko ya Tabia Nchi, Margareth Nzuki kwa pamoja wakiwa wamenyanyua kitabu cha Mwongozo wa Mafunzo ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo, Elimu ya Ujasiriamali na Stadi za Biashara mara baada ya kuzinduliwa na mgeni rasmi kwenye mafunzo ya siku moja Juu ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika (SACCOS na VICOBA) na Maafisa Ushirika wa kutoka Wilaya za Bunda, Bukoba na Sengerema yaliyoandaliwa na ESRF na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza.
IMG_6627
Lungu Phares kutoka SELF Micro finance Fund akielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa taasisi ikiwemo utoaji mikopo wenye masharti nafuu.
IMG_6215
Dkt. Jones Kaleshu kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi akiwasilisha mada ya hali ya Ushirika ya kuweka na kukopa nchini;changamoto na fursa zilizopo katika mafunzo ya siku moja juu ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo kwa Viongozi wa Vyama vya Akiba na Mikopo pamoja na Maafisa Ushirika wa Wilaya iliyoandaliwa na ESRF na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo UNDP yaliyofanyika jijini Mwanza katika Hoteli ya Malaika Beach Resort.
IMG_6200
Baadhi ya washiriki wakijadiliana jambo wakati wa uwasilishaji wa mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mafunzo hayo.
IMG_6568
Afisa Ushirika wa Bunda, Saulo Lunyeka akiwasilisha ya Utawala wa Majanga na Usimamizi wa Akiba na Mikopona Umuhimu wake kwa wananchama wa jamii; umuhimu wa kukuza mitaji.
IMG_6523
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya Ilemela, Manju Msambya aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (wa nne kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa nne kulia), Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon Manyama (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Mawasiliano wa ESRF ambaye pia ni Mratibu wa mradi wa Kukuza Uchumi, Kuleta Maendeleo Endelevu Kupitia Utunzaji Mazingira, Usawa wa Kijinsia na Kupunguza Mabadiliko ya Tabia Nchi, Margareth Nzuki (kushoto) katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku moja juu ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo kwa Viongozi wa Vyama vya Akiba na Mikopo pamoja na Maafisa Ushirika wa Wilaya yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
IMG_6528
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya Ilemela, Manju Msambya aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (wa nne kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa nne kulia), Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Amon Manyama (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Mawasiliano wa ESRF ambaye pia ni Mratibu wa mradi wa Kukuza Uchumi, Kuleta Maendeleo Endelevu Kupitia Utunzaji Mazingira, Usawa wa Kijinsia na Kupunguza Mabadiliko ya Tabia Nchi, Margareth Nzuki (kushoto) katika picha ya pamoja na Wanawake Viongozi wa Vyama vya Akiba na Mikopo pamoja na Maafisa Ushirika wa Wilaya.

No comments:

Post a Comment