Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, November 22, 2015

SKYLIGHT WAZIDI KUWASHA MOTO NDANI YA ESCAPE ONE NJOO LEO UONE MAMBO MAPYA KUTOKA KWENYE BENDI HII

Sony Masamba akiongoza marapa wenzake wa Skylight Band, Sam Mapenzi   na Joniko Flower kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Jumapili iliyopita ndani ya kioa cha Escape One Mikocheni ambapo leo pia burudani iko pale pale na ndio kwanza week end imeanza kwa fans wa Skylight Band.
Kifaa kipya cha Bandi ya Skylight, Leah pamoja na  Suzy wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita sasa leo sio siku ya kukosa njoo ujionee mambo mapya kutoka kwenye bandi ya Skylight
Mashabiki wakicheza kwa kuzungusha duala hapa ni kukata mauno mpaka kieleweke.
Shabiki mzalendo wa Skylight Band, Miryam Kamaliza (kushoto) akipata Ukodak na  rafiki yake ndani ya kiota cha Escape One.

 
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiimba akiimba huku wasanii wa bendi hiyo pamoja na mashabiki wakiendelea kuselebuka na mziki mzuri kutoka Skylight.
Waimbaji wa Bendi ya Skylight wakiendelea kutoa burudani huku wakiongozwa na Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi wa Skylight Band, Joniko Flower
Joniko Flower akichana mistari huku waimbaji wa bendi hiyo wakiendelea kuerebuka na shabiki wa Skylight Band Jumapili iliyopita kwenye kiota cha Escape One.
Kasongo Junior na Suzy wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita, bila kukosa ya leo itakuwa pale pale.
Sam Mapenzi akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Jumapili iliyopita ndani ya kioa cha Escape One Mikocheni ambapo leo pia burudani iko pale pale na ndio kwanza week end imeanza kwa fans wa Skylight Band.

Wapenzi wa kweli wa Bendi ya Skylight wakiwa kwenye ukodaki wakati bendi hiyo ikiendelea kutoa burudani ndani ya Kiota cha Escape One jijini Dar
Hakika kwenye shoo ya Skylight ya kila Jumapili sio ya kukosa njoo ujionee mambo mazuri kutoka katika bendi ya Skylight.....Just Follow the Light.
Mwimbaji wa Bendi ya Skylight Suzy  akiendelea kuwakonga nyoyo mashabiki wa bendi hiyo uku akisindikizwa na Kasongo Junior na Sony Masamba ndani ya kiota cha Escape One Mikocheni
Mashabiki wakiendelea kujimwaga na burudani ya Skylight Band kiota cha Escape One.

No comments:

Post a Comment