Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 14, 2015

DEREVA MZEMBE AHUKUMIWA MIAKA MITATU JELA MKOANI MBEYA

Na Ezekiel Kamanga ,Mbeya
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya imememhukumu kwenda jela miaka mitatu Martin Mhina Dereva wa basi la Majinja kwa kuendesha gari kwa uzembe.
Waendesha Mashitaka wa Serikali Hannarose Kasambala na Catherine Gwatu wameiambia Mahakama kuwa Dereva huyo aliendesha Basi la Kampuni ya Majinja kwa uzembe mapema mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi kwa kuigonga gari aina ya Toyota Hilux na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Mawakili hao wameiambia Mahakama kuwa Kesi hiyo namba 46/2015 ambapo Dereva huyo alitenda kosa hilo kinyume 


cha Sheria ya usalama barabarani namba 40(1),63(2)(a),27(1)(a)III(c) kifungu cha 168 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Akijitetea mbele ya Mahakama Martin ameiomba Mahakama kumsamehe kwa kuwa hilo ni kosa lake la kwanza na kwamba anayo familia inayo mtegemea hivyo imwonee huruma kutokana na kosa hilo.

Baada ya kupitia ushahidi uliotolewa Mahakamani na Upande wa Mashitaka na utetezi wa Mshitakiwa Hakimu Zawadi Laizer alimtia hatiani kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela ili iwe fundisho kwa madereva wasifuata sheria za usalama barabarani.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment