Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, December 3, 2015

LIPUMBA NA WENZAKE WAACHIWA HURU
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Profesa Ibrahim Lipumba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF na wafuasi 30.
Hakimu Mkazi Mkuu, Shaidi Huruma jana aliwaachia huru washtakiwa hao baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi kwa niaba ya Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kuwasilisha hati chini ya kifungu 91 (1) cha sheria ya Makosa ya Jinai sura ya 20 akiomba kesi hiyo iondolewe mahakamani hapo kwa sababu hawana nia ya kuendeleza mashtaka dhidi yao.
Baada ya kuwasilishwa kwa hati hiyo ya DPP, Hakimu Huruma alisema kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka hana nia ya kuendeleza mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili aliwaachia huru na kuwatakia maisha mema.
Mbali na Lipumba, wafuasi 30 wa Chama cha Wananchi (CUF) walioachiwa huru ni Shabani Ngurangwa (56), Shabani Tano au Kasakwa (29), Shabani Polomo (40), Juma Mattar (54), Mohammed Kirungi (40), Athumani Ngumwai (40), Shaweji Mohamed (39) na Abdul Juma (40).
Wengine ni Hassan Saidi (37), Hemed Joho (46), Mohamed Mbarucu (31), Issa Hassani (53), Allan Ally (53), Kaisi Kaisi (51), Abdina Abdina (47), Allawi Msenga (53), Mohamed Mtutuma (33) na Salehe Ally (43).
Pia wamo Abdi Hatibu (34), Bakari Malija (43), Abdallah Ally (32), Said Mohamed (40), Salimu Mwafisi, Saleh Rashid (29), Abdallah Said (45), Rehema Kawambwa (47), Salma Ndewa (42), Athumani Said (39), Dickson Leason (37) na Nurdin Msati (37).

 
Kwa pamoja wanadaiwa kula njama za kufanya uhalifu, kufanya mkusanyiko usio halali na kufanya mgomo baada ya makatazo halali ya Polisi.
Ilidaiwa kuwa Januari 27, 2015 maeneo ya wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote wanadaiwa kuwa walikuja njama ya kufanya uhalifu.
Mshtakiwa wa kwanza hadi wa 28, wanadaiwa siku hiyo katika ofisi za CUF, karibu na Hospitali ya Temeke, bila halali walifanya mkusanyiko kwa nia ya kufanya maandamano yasiyo halali kwenda viwanja vya Mbagala Zakhem.
Kabla ya kufutwa kesi ilikuwa katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka na ilipangwa kuendelea kwa usikilizwaji Januari 5,2015.
Ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha na Wakili wa Serikali Mkuu, Benard Kongola.
Awali akitoa ushahidi katika kesi hiyo, Mkuu wa Operesheni Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Simon Siro (54) kuwa walipiga marufuku maandamano na mkutano uliotaka kufanywa na CUF Januari 27,2015 kutokana na taarifa za intelijensia za kuwapo kwa tishio la ugaidi.
Alidai Januari 23 mwaka huu walipokea barua ya CUF ikiiarifu polisi kuwa Januari 27 mwaka huu wangefanya mkutano na maandamano yenye lengo la kukumbuka watu waliouawa Pemba na kulaani mauaji hayo.
Siro, barua hiyo ya CUF ilidai kuwa chama hicho kimekuwa na tabia ya kuwakumbuka watu waliouawa na kuyalaani mauaji hayo kila mwaka, Januari 27.
Maandamano hayo ya Januari 27, mwaka huu yalianzia katika ofisi za CUF Temeke yakiongozwa na Lipumba kuelekea viwanja vya Zakhem kwa ajili ya mkutano wa hadhara.

CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment