Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, December 26, 2015

MAMBO SAFI KWA SAMATTA...ANAKWENDA KATIKA TIMU HII YA ULAYA,INASHIKA NAFASI YA SITA ..HATA KIPA WA CHELSEA KATOKEA HAPO

Headlines za mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta zinazidi kushika kasi, Samatta anatajwa kuwa katika mpango wa kwenda kucheza soka la kulipwa barani Ulaya,mara tu dirisha dogo la usajili la mwezi January litakapofunguliwa.
Generated by IJG JPEG Library
Samatta akionesha uwezo wake katika mechi ya robo fainali ya klabu Bingwa Dunia
Headlines ambazo zimenifikia kutoka katika mtandao wa www.voetbalkrant.com zinaripo nyota huyo tegemeo wa watanzania kuwa katika mipango ya kwenda kucheza soka katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Samatta anatajwa kuandikwa na mitandao ya Ubelgiji kujiunga na klabu hiyo.

 
samatta
Hii ndio taarifa iliyoandikwa na mtandao wa www.voetbalkrant.com kuhusu Samatta kuhitajika na klabu ya KRC GENK
Samatta ambaye anatajwa kuwa na rekodi ya kucheza jumla ya mechi 103 na kufunga jumla ya magoli 60 toka ajiunge na TP Mazembe mwaka 2011 kwa mujibu wa www.voetbalkrant.com, anatajwa uwezo wake kumvutia mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya KRC Genk Dimitri De Conde.
KRC Genk ambayo msimu huu inatajwa kuwa na safu mbovu ya ushambuliaji, mwaka 2012 ilishiriki na kuingia katika hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Ulaya, klabu ya KRC Genk (Racing Genk) ndio klabu iliyomuuza kiungo wa sasa wa Man City Kevin De Bruyne na golikipa namba moja wa sasa wa Chelsea Thibaut Courtois kwenda Chelsea mwaka 2012. Kwa sasa klabu hiyo ipo nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji.
sama
Msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji ikiionesha klabu ya KRC GENK ambayo imeandikwa Racing Genk ikiwa nafasi ya sita katika Ligi.

No comments:

Post a Comment