Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 21, 2015

ORODHA YA WAUZA DAWA ZA KULEVYA HAINISADII-KITWANGA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mazungumzo na Viongozi Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini. Waziri Kitwanga aliwaambia waandishi wa habari kuwa, wamekubaliana na Viongozi Wakuu wa jeshi hilo kuweka mikakati zaidi ya kukabiliana na uhalifu nchini. Wapili kushoto meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Wapili kulia meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki. Kulia ni Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo, Paul Chagonja. Kushoto meza kuu ni Kamishna wa Polisi Jamii nchini, Mussa Ali Mussa. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova.


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAZIRI wa Mambo Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema njia ya kudhibiti dawa za kulevya kuingia nchini ni kuweka mfumo wa kisasa wa kudhibiti uingiaji dawa hizo, kuwa na orodha ya waingizaji wa dawa ni kazi bure kutokana na kukosa mamlaka ya kisheria.
Kitwanga ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Maafisa Wakuu wa Jeshi la Polisi, amesema katika kukabiliana na uingizaji wa dawa za kulevya ni kuweka mfumo imara na jeshi la polisi lazima lijipange katika udhibiti huo.
Kitwanga amesema kuwa mfumo wa kiteknolijia ukiwekwa hautabagua mtu yeyote au mkubwa katika madaraka awe mdogo wakishajulikana watachukuliwa hatua za kisheria bila kuangaliwa nafasi walizo nazo.
“Orodha ya wauza unga ukiwanayo haitasaidia na kufanya hivyo ni kuhisi, lakini huna sheria ya kuweza kuwabana katika orodha hiyo” amesema Kitwanga.
Kitwanga amesema kuwa katika mambo waliyojpanga nayo na jeshi la polis ni kuhakikisha wanaimarisha ulinzi katika bandari ili kuweza kudhibiti utoroshaji wa vitu mbalimbali ambavyo vinatoka bila utaratibu.
Hata hivyo amewataka polisi watu washitakiwe kwa kesi walizo nazo na sio kuwabambikia watu wasio na hatia kusababisha kufungwa kwa kesi zisizowahusu.
Kitwanga amesema utoroshaji wa madini,jeshi la polisi haliwahusu wakihitajika na Wizara ya Nishati na Madini watafanya hivyo katika kukabiliana na utoshaji huo.
Aidha amesema kati ya askari 45,000 ni askari 10,000 ndio wenye makazi hivyo wanatarajia kujenga nyumba 5000 ikiwa nia nia askari wote kukaa katika makambi ni rahisi kuweza kuhitajika kwa muda wowote.

No comments:

Post a Comment