Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 28, 2015

PICHA 8:::DIAMOND PLATINUMS AANGUA KILIO DAR LIVE KISA HIKI HAPA.



 

Musa mateja
SIYO sinema! Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amejikuta akiangua kilio kama mtoto mdogo na kuwashangaza watu kufuatia mashabiki wake kumtaka awaimbie ‘akapela’ ya wimbo wake mpya wa Utanipenda, twende na Ijumaa Wikienda.
Tukio hilo ambao bado limo midomoni mwa mashabiki wake, lilijiri usiku wa kuamkia Boxing Day (Desemba 26, 2015) ndani ya ‘Uwanja wa Taifa wa Burudani’ Dar Live jijini Dar ambapo nyota huyo alikuwa akikamua jukwaani na shoo ya nguvu iliyopewa jina la Funga Mwaka Concert.
DAKIKA CHACHCE KABLA YA KULIA
Dakika chache kabla Diamond hajamwaga chozi, mashabiki wake walimuomba aimbe ‘akapela’ ya wimbo huo mpya ambao ndiyo habari ya ‘mujini’ kwa sasa.
Wakati akiimba akapela hiyo, mashabiki wake, bila kificho, walimwambia anajitabiria ‘kufulia’ kwani wimbo huo una kila alama za yeye kumaliza gemu la Bongo Fleva vibaya.



MASHABIKI WALICHANGIA?
Hata hivyo, licha ya mashabiki kumpasulia hivyo, baadhi yao walianza kulia wakionekana kuguswa na mashairi ya wimbo huo hali iliyosababisha Diamond naye aanze kulia na kushindwa kuendelea kuuimba wimbo huo.
DADA’KE AMTOA JUKWAANI
Kufuatia hali hiyo, dada yake kwa upande wa baba yake, Abdul Jumaa, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ alimfuata jukwaani na kumtoa huku akimfunika na kitambaa cha bendera ya taifa ambacho pia dada huyo alikitumia kumfutia machozi kaka yake huyo.
NYUMA YA JUKWAA
Diamond alipelekwa nyuma ya jukwaa ambako ukiachia mbali yeye Queen Darleen, meneja wake, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ naye alitumia nguvu ya ziada kumbembeleza staa huyo huku akimwambia anawapa wasiwasi mashabiki wake. Kwa hiyo anyamaze.



AAA WAPI!
Licha ya Babu Tale kutumia hekima ya kibabubabu, bado Diamond aliendelea kulia, safari hii kwa uchungu zaidi na kujiinamia huku akikataa kutulizwa wala kuambiwa maneno yoyote yanayoonekana ‘kama’ yana busara ndani yake.
“Huna sababu ya kuendelea kulia ndugu yangu kwani kufulia au kuendelea kuwa na mali ni neema na msimamo wa Mungu. Hakuna binadamu anayeweza kumshusha mwenzake kama Mungu hajapanga kuwa hivyo,” alisema Babu Tale lakini Diamond hakumsikiliza.

Diamond alinyamaza mwenyewe baadaye kufuatia mawasiliano ndani ya ubongo wake kumwambia ‘umelia sana kijana, imetosha sasa’!
SHOO IKAWA IMEISHA
Kilio hicho, kilimaliza shoo hiyo kwani Diamond hakurudi tena jukwaani baada ya kukamua nyimbo zake kibao na kuwafanya mashabiki wake kuiweka siku hiyo katika kumbukumbu.
SHABIKI ASIMULIA KUGUSWA KWAKE
Naye shabiki mmoja ambaye hakutaja jina, alizungumza na gazeti hili kufuatia Diamond kumaliza shoo kwa kulia:
“Dah! Nimeguswa na wimbo wa Diamond kiasi kwamba hata mimi mwenyewe nimejikuta nikilia kama ilivyomtokea jamaa. Inaonekana anajua kutunga sana.
“Unajua kilichomfanya Diamond alie ni namna alivyowaona mashabiki wake wakihuzunika baada ya kuanza kuimba akapela yake.”

Juzi, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Diamond na kumuuliza kisa cha kulia vile ambapo alisema:
“Mwana ile hali huwa inatokea. Unajua wimbo wenyewe unanigusa mimi katika kila hatua. Nilijiuliza, iko siku nitakwenda Dar Live kuimba halafu nikakosa watu? Iko siku kumbe mimi nitakuwa si kitu tena, sitapendwa!”

No comments:

Post a Comment