Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, December 4, 2015

Spika Ndugai aongoza maelfu kuuaga mwili wa Mkurugenzi wa BungeMarehemu Hellen Stephen Mbebha wakati wa uhai wake.
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) akiweka shada la maua juu ya kaburi la aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Shughuli za Bunge Marehem Hellen Mbebha.
Katibu wa Bunge la Tanzania Dkt. Thomas Kashilillah akitoa heshima za mwisho kwa kwa mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Shughuli za Bunge Marehem Hellen Mbebha ambapo mazishi yake yalifanyika katika kijiji cha Kung’ombe wilayani Bunda mkoa wa Mara tarehe 01/12/2015. Aliyesimama ni Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge Bi. Nenelwa Wankanga.

 
Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge Mhe. Kangi Lugola na Mhe. Abdulkadir Shah wakiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Hellen Mbebha.
Watoto wa marehemu Helen Mbebha, Nassoro na Nasra, wakiwa na Babu na Bibi yao wakati wa mazishi ya mama yao kipenzi.
Mama mzazi wa marehemu Hellen Mbebha akiwa hajiwezi wakati wa kuusindikiza mwili wa binti yake makaburini huko Wilaya ya Bunda kijiji cha Kung’ombe.
Mhe. Rose Kamili (Mb) akiongoza wabunge wanawake kuweka shada la maua juu ya kaburi la marehemu Hellen Mbebha.
Hii ndyo ilikuwa safari ya mwisho ya marehemu Hellen Mbebha hapa duniani. BWANA alitoa, BWANA alitwaa. Jina la BWANA na lihimidiwe. Amina (Picha na Prosper Minja – Bunge)

No comments:

Post a Comment