Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 14, 2015

TRAFFIC MWANZA ATUMBUKIZA BAJAJI DEREVA WA BODABODA MTARONI


Kupitia kipindi cha KAZI NA NGOMA ya JEMBE FM Mwanza stori ya Traffic aliyetumbukia mtaroni akiendesha bajaji ya mizigo aliyoikamata kutoka kwa dereva wa bodaboda imesikika, nini kisa na mkasa kwa ufupi ni kwamba> Mara baada ya kumkamata mwendeshaji Hamisi Omary kwa kosa la kupakia mzigo mkubwa wa mbao alimwamuru kulipa faini ya shilingi elfu 30, naye Hamisi akamwomba msamaha kwa Traffic huyo kwamba ni fedha nyingi sana ambayo hawezi kuilipa kwa hata kipato anachokipata toka kwa tajiri aliye mpa mzigo kuusafirisha toka eneo moja hadi jingine.

Traffic huyo akauliza kuhusu leseni, dereva huyo akaonyesha,....leseni ya biashara akaonyesha.... Traffic huyo alipoona hakuna kosa jingine akarudi kwenye kosa la kwanza, akitumia kauli ya "Siwezi kukusamehe, nakulipua huku nacheka"   
Mwendeshaji Hamisi Omary akizungumza nasi kilichotokea.
Traffic huyo mwenye namba (Zimehifadhiwa) kuitumbukiza bajaji hiyo mtaroni.
Wananchi wakisaidiana kuitoa bajaji hiyo mtaroni mara baada ya mvutano wa mabishano kutaka michoro ya usalama barabarani ifanywe na matraffic waliokuwa zamu kutokea na hatimaye kufanyika.

Bajaji yenye namba....
Eneo la ajali ni kiunganishi cha barabara ya Makongoro Airport na kushuka Uwanja wa CCM Kirumba, karibu na Mwanza City Mall, lilizungukwa na wadau wa bodaboda.

Kwa sasa mkoani Mwanza na maeneo mbalimbali nchini kuna baadhi ya sura mpya za wanausalama wa vyombo vya usafiri barabarani ambapo licha ya wale wakongwe waliohamishwa toka mkoa mmoja kwenda mwingine pia kuna wapya waliotoka vyuo vya jeshi nchini. 

Swali kuu ni>Je? baadhi ya wadau hawa wa usimamizi wa usalama wa vyombo vya usafiri barabarani wanazisimamia kweli sheria ipaswavyo, Je? wanafanya kazi zao vipi na kwa hali gani, kwa nia ya kuonya, kuelimisha au kukomoa?

No comments:

Post a Comment