Sehemu inayoendelea kufukiwa hapo Mtoni Marine ambayo itatumika hapo baadae kwa ajili ya eneo maalum litakalotoa fursa kwa Wananchi kupata mapumziko.{ Public Beach }.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar { ZIPA } Nd. Salum Khamis Nassor akimueleza Balozi Seif hatua zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kuona taratibu za uwekezaji zinachukuliwa kwa wanaowekeza vitega uchumi vyao Nchini.
MRADI mkubwa wa Kimataifa wa ujenzi wa kisiwa cha Kitalii ambacho kitatengenezwa kwa mfumo wa ufukiaji Bahari umeanza rasmi katika eneo la Hoteli ya Utalii iliyopo Mtoni Marine kaskazini Magharibi ya Mji wa Zanzibar.
Hata hivyo gharama kamili za Mradi huo bado hazijafahamika wakati utakapokamilika rasmi ujenzi wake hapo baadaye.
Mradi huo unaoendeshwa na Kampuni ya Kizalendo ya Baghresa Group utahusisha ujenzi wa Hoteli ya Kimataifa ya Ghorofa Tano ya Daraja la Tano { Five Star + }, utengenezaji wa eneo la wazi la mapumziko { Public Beach } pamoja na kutengeneza Kisiwa cha Mji mpya.
No comments:
Post a Comment