Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, December 31, 2015

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ampongeza Mbwana Samatta kwa kujiunga na klabu ya Genk ya Ubelgiji

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(kushoto) akiongea na Mchezaji wa Timu ya TP Mazembe Mbwana Samatta(kulia) jana jijini Dar es salaam.Mbwana amemtembelea waziri Nape ofisini kwake na kuomba baraka za wizara katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani na pia kumpa habari njema za yeye kutegemea kujiunga na timu ya Ubelgiji ya Genk.
Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(katikati)akiongea na waandishi wa Habari na kuwaomba watanzania kumwombea Mbwana Samatta ili ashinde katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani kwani ni jambo la Taifa zima.Mhe Nape pia alimhakikishia kuwa Serikali ipo nyuma yake na ipo katika mkakati wa kuifanya michezo kuwa Shughuli Rasmi kwani itawafaidisha wanamichezo na Serikali kwa kupata kodi. 

 

Mchezaji wa TP Mazembe Mbwana Samatta(wa kwanza kushoto)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) sababu za yeye kumtembelea Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika ofisi ya Wizara hiyo.Mbwana alisema kuwa amemtembelea waziri uyo kwa ajili ya kumfahamisha kuwa yumo katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani na hivyo kuomba baraka za Wizara.Pia kumpongeza Mhe. Nape kwa kuchaguliwa kuwa waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.Mbwana anategemea kujiunga na klabu ya Mpira ya Genk ya Ubelgiji kwa mkataba wa miaka minne.
Picha na Daudi Manongi-WHUSM.

No comments:

Post a Comment