Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, January 13, 2016

AKAMATWA NA MENO YA TEMBO KILO 50 YENYE THAMANI YA TSH MIL 120 MKOANI KATAVI

Meno ya Tembo vipande 8 vyenye uzito wa kilo 50 ya thamani ya milioni 120 ambayo ni sawa na Tembo hai wane aliyokamatwa nayo hivi karibuni mtuhumiwa Nzuri Ndizu Mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
Mtuhumiwa Nzuri Ndizu Mkazi wa Kijiji cha Mbende Wilaya ya Mlele akiwa katika ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi baada ya kukamatwa na meno ya Tembo vipande nane yenye thamani ya shilingi milioni 120 hapo juzi 


.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa Katavi Dhahiri Kidavashari akiwa ameshika meno ya Tembo aliyokamatwa nayo mtuhumiwa Nzuri Ndizu mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi ambae alikamatwa juzi akiwa na vipande 8 yenye thamani ya milioni 120 .

Picha na Walter Mguluchuma Katavi yetu blog

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Nzuri Ndizu (44) Mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi amekamatwa akiwa na meno ya Tembo nane yenye uzito wa kilogramu 50 yakiwa na thamani ya shilingi milioni 120 ambapo ni sawa na Tembo wanne waliuwawa.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa mida ya saa tatu na nusu .

Kidavashari alisema mtuhumiwa Ndizu alikamatwa kufuatia misako na uparesheni mbalimbali zinazoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi ikiwa ni kuhakikisha wahalifu wa makosa mbalimbali wakimemo wawindaji haramu wa wanyama pori wanakamatwa.Siku hiyo ya tukio jeshi la polisi lilipata taarifa toka kwa Raia wema kuwa katika pori la akiba la Lwafe kuna watu wanajihusisha na biashara haramu ya meno ya Tembo .

Kidavashari aliendelea kuwaambia waandishi wa Habari baada ya taarifa hizo kupokelewa ufuatiliaji ulifanyika kwa polisi kufika kwenye eneo hilo na kuweka mtego .Na walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Nzuri Ndizu akiwa na meno ya Tembo vipande nane akiwa ameyaficha kwenye pori kwa ajiri ya kusubilia wateja .

Kamanda Kidavashari alisema mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi kwa hatua za upelelezi zaidi ilikuendelea kubaini mitandao yote inayojihusisha na biashara hiyo haramu ya meno ya Tembo na kufikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika .

Hivi karibuni watu watatu walikamatwa katika mtaa wa Aiter Mjini hapa wakiwa na vipande kumi na mbili vya meno ya Tembo yenye thamani ya shilingi milioni 120 hari hiyo inaonyesha kuwa kuna kasi kubwa ya biashara haramu ya meno ya Tembo Mkoani Katavi .Na Katavi yetu blog/Blogs za Mikoa

No comments:

Post a Comment