Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, January 21, 2016

GAZETI LA JAMHURI LAPEWA SIKU SABA KUKANUSHA HABARI YA FAMILIA YA JK KUHUSIKA NA UDA

Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Simos Group na UDA, Robart Kisena akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii
GAZETI la Jamhuri lapewa siku saba kukanusha habari iliyoandikwa kwenye gazeti hilo Januari 18, 2016 toleo no. 25  lililokuwa na kichwa cha habari FAMILIA YA JK  YAHUSIKA UDA habari iliyokuwa ukurasa wa mbele wa gazeti hilo.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Simos Group na UDA, Robart Kisena wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,amesekuwa hakuna uhusiano wa umiliki na familia ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne,Dk Jakaya Kikwete.
Kisena amesema kuwa Familia ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete hahusiki kabisa kwani kampuni ya UDA na kampuni ya Simon Kisena haihusiani na familia ya JK hata miradi inayofanywa na Kampuni hiyo.Aidha  amesema gazeti lililoandika habari hiyo linatakiwa kuomba radhi kwa siku hizo kwa kuwa na  habari yenye uzito ule ule na ukurasa ule ule.
Kisena amesema  wasipofanya hivyo watapelekwa mahakamani ili wakatoe ushaidi wa maandishi mahakamani hapo juu ya uhusikaji wa Familia ya Rais Mstaafu katika kampuni ya usafiri Dar es Salaam (UDA).
Hata hivyo amesema  kuwa kampuni ya (UDA) itarudishwa  kwa wananchi ifikapo Machi Mwaka huu ili iweze kuendeshwa kwani shirika hili kwa mara ya kwanza lilikua na magari 7 mpaka sasa maari hayo yameongezeka na kufikia zaidi ya magari 400.

No comments:

Post a Comment