Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na kufanya usafi katika Mtaa wa Gongo la Mboto Manispaa ya Ilala, Ali Mwinyimkuu (kulia), akishiriki kufanya usafi na wananchi Dar es Salaam jana, ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kufanya usafi kila baada ya wiki mbili ili kuunga mkono kauli Rais Dk. John Magufuli ya kufanya usafi katika maeneo tunayoishi na kufanyia shughuli zetu nchini.
Kazi ya usafi ikiendelea.
Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na kufanya usafi katika Mtaa wa Gongo la Mboto Manispaa ya Ilala, Ali Mwinyimkuu Omari akiwaongoza wenzake kufanya usafi.
Hapa ni kazi tu tunaukataa uchafu.
Wanawake wakishiriki kufanya usafi eneo la relini.
Mwenyekiti wa Mtaa huo, Bakari Shingo (Aliyevaa kaputura), akishiriki kufanya usafi na wananchi wake Dar es Salaam jana, ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kufanya usafi kila baada ya wiki mbili ili kuunga mkono kauli Rais Dk. John Magufuli ya kufanya usafi katika maeneo tunayoishi na kufanyia shughuli zetu nchini.
Usafi ukiendelea.
Wasanii wa Kikundi cha Rock Star wa Mtaa huo nao walishiriki kufanya usafi.
Na Dotto Mwaibale
WANANCHI wa Mtaa wa Gongolamboto Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameendelea kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kufanya usafi katika eneo hilo kwa wiki mara mbili ili kuyaweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea mtaa huo Dar es Salaam jana kujionea shughuli za usafi katika eneo Mwenyekiti wa mtaa huo Bakari Shingo alisema lengo lao kubwa ni kuiunga mkono kauli ya Rais Magufuli ya kufanya usafi ambapo wao wameamua kufanya usafi kwa wiki mara mbili.
Alisema lakini wao walianza kufanya usafi katika eneo kabla ya rais kuanza kuhimiza lakini kauli ya Magufuli ilichochea zaidi moto wa kufanya usafi kwa wananchi wa eneo hilo.
Shingo alisema katika mtaa wao kunavikundi ambavyo vinasaidia kufanya usafi ambapo wamegawa maeneo na utaratibu huo umesaidia kuyaweka mazingira katika hali ya usafi.
Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na usafi katika mtaa huo Ali Mwinyimkuu Omari alisema kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa katika suala zima la usafi katika eneo hilo kutokana na utaratibu waliojiwekea.
Alisema wanamshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Issaya Mngulumi kwa kujitoa kwake kuwapa gari la kusomba takataka kila wanapofanya usafi hali ambayo inawapa moyo wananchi wa kufanya usafi hivyo kumungana mkono Rais Dk. John Magufuli katika suala zima la usafi nchini.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment