Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, January 15, 2016

MUME WA MWANAMUZIKI CELINE DION AFARIKI DUNIA


Rene Angelil, mume wa mwanamuziki mashuhuri duniani Celine Dion, amefariki dunia siku ya Alhamisi (Jan 14) huko nyumbani kwao Las Vegas baada ya kuugua saratani, mwanamuziki huyo ametangaza.
Bw Angelil, aliyemuoa Dion mwaka 1994 na wakajaliwa kupata watoto watatu, amekuwa pia akifanya kazi kama meneja wa mwanamuziki huyo mkongwe.
Dion alichukua likizo kutoka kwenye muziki kwa vipindi 


viwili ili kumuuguza Angelil baada ya kupatikana na saratani ya koo mwaka 2000.
Bw Angelil alizaliwa mjini Montreal mwaka 1942 na amefariki akiwa na miaka 73.

No comments:

Post a Comment