Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, January 28, 2016

MWANAMITINDO, FLAVIANA MATATA AZINDUA RANGI YA KUCHA JIJINI DAR

Mwanamitindo wa Tanzania ambaye anafanya kazi za mitindo nchini Marekani, Flaviana Matata amezindua bidhaa za  urembo za kucha zinazojulikana kwa jina la LAVY, amezindua bidhaa hiyo mbele ya waandishi wa habari na kuomba wanawake na watumiaji rangi za kucha  wamuunge mkono kwani ni bidhaa ambayo ipo kwenye soko kwa kipindi hiki kwani kila mwanamke anapenda kupendeza. Kulia ni Afisa mtendaji mkuu wa Shear Illution  Ltd, Shekha Nasser akiwa ni mmoja wa wasambazaji wa  kipodozi cha Kucha ambazo zimezinduliwa.
Wakati huhuo amewapongeza wote waliochangia katika kufanikisha yey kujulikana kimataifa.
Afisa mtendaji mkuu wa Shear Illution  Ltd, Shekha Nasser  akizungumza na waandishi waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na kushirika katika uuzaji wa vipodozi vya kucha ambavyo vitakuwa kikiuzwa katika duka lake.

 
Bidhaa za kucha zinazojulikana kwa jina la LAVY  amazo zimezinduliwa na mwanamitindo Flaviana Matata jijini Dar es Salaam.
Bidhaa hizo zitakuwa zikipatikana kwenye maduka mbalimbali na Saluni za Pikasso, Shear Illution  Ltd na Zuri Cosmestics zilizopo jijini Dar es Salam kwa shilingi elfu tano tuu.

No comments:

Post a Comment