Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, January 5, 2016

MWIGULU NCHEMBA ATIMUA VIGOGO WALIOKULA BILION 5.7 ZA UJENZI WA MACHINJIO YA KISASA RUVU

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi akiwasili kwenye mradi uliodumaa wa Ujenzi wa machinjio ya kisasa wa ranchi ya Ruvu .Sehemu ya jingo lililobaki kama Gofu mara baada ya kutelekezwa na Uongozi wa Bodi ya ranchi za Taifa(NARCO)Mwigulu Nchemba akishangaa namna mali hii ya Umma ilivyotekelezwa.

 
Mwigulu akiwa na jopo la wataalam wakiendelea kutathimini hasara iliyojitokeza kutokana na ujenzi mbovu wa machinjio ya kisasa hapa Ruvu.
Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Chalinze Mh.Ridhiwani wakisikiliza kwa makini sababu zilizopekea jingo hilo kutelekezwa.Anayetoa maelezo wa mwisho kushoto ni msimamizi wa ranchi hiyo Ngd.Bwire.

Sehemu ya jingo ikiwa imetelekezwa bila kuendelezwa kiujenzi.Hii ni sehemu ya ukuta wa jingo hilo ambao umekatika kutokana na kukaa muda mrefu bila kuendelezwa.Mwigulu Nchemba akiendelea kupewa maelezo ya kina kuhusu ubadhilifu uliojitokeza kwenye ujenzi huu.Mh.Ridhiwani kikwete Mbunge wa Chalinze akitoa malalamiko yake kwa Waziri.Mwigulu Nchemba kuhusu kukosekana kwa mahusiano mazuri kati ya wamiliki wa ranchi na wananchi wanaozunguka ranchi ya Ruvu.Kwa mbali hili ndio jengo la machinjio ya kisasa lililokuwa linajengwa na hatimaye kutelekezwa bila kuendelezwa tangu mwaka 2010.Mh:Mwigulu Nchemba akiteta jambo na viongozi wanaohusika na kulinda baadhi ya vifaa vilivyonunuliwa kwaajili ya ranchi hiyo ya kisasa.Mh;Mwigulu Nchemba akioneshwa baadhi ya Ng'ombe wanaopatikana kwenye ranchi hiyo.Mwigulu Nchemba akiwa kazini kwenye shamba la Mifugo la Ruvu hii leo.Mwigulu Nchemba akidadisi utunzaji wa maji ya Mifugo inayopatikana ndani ya ranchi ya Ruvu.
---
Wakati Taifa na Mataifa yakiendelea kutoa pongezi zao kwa serikali ya Rais Magufuli kwa speed yake ya uchapa kazi,Mawaziri wake pia wameendelea kuonesha namna walivyodhamiria kusimamia shughuli za maendeleo ya Nchi yetu.

Hii leo,Mh:Mwigulu Nchemba mwenye dhamana ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi amefanya ziara ya siku moja kwenye ranchi ya Taifa ya Ruvu kukagua ujenzi wa majengo ya machinjio ya kisasa ulioanza mwaka 2010.

Katika hali ya kusikitisha na kulazimu kuchukua hatua za kinidhamu,Mwigulu Nchemba amekutana na ubadhilifu wa Bilioni 5.7 ambazo zilitolewa kwaajili ya ujenzi wa jengo hilo,Fedha hizo zilizokuwa zimelengwa kuwezesha ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa hazijafanya kazi kama ilivyokusidiwa.

Waziri huyo wa kilimo amekuta mradi huo umetelekezwa tangu mwaka 2010 bila kuendelezwa,Sababu za kutelekezwa kwa mradi huo zikidaiwa kuwa ni kutofautiana kwa mkandarasi na bodi ya NARCO(kampuni ya usimamizi wa ranchi za Taifa) hazikukubalika na Mh: Mwigulu Nchemba ambaye baada ya kusikiliza kwa makini ufafanuzi wa kutoka kwa viongozi wa ranchi hiyo aliamua ifuatavyo.

Kwanza,Mwigulu Nchemba amewatimua wakurugenzi wote wa bodi ya NARCO yenye dhamana ya kusimamia ranchi za Taifa kwa kushinda kukamilisha ujenzi wa mradi huo.Mbali na kushindwa,bodi hiyo imeutelekeza mradi huo na hivi sasa inapendekeza kujengwa kwa mradi mwingine kama huo ndani ya eneo hilohilo la ranchi ya ruvu.

Pili, Mwigulu Nchemba amesitisha utumishi wa Mkurugenzi mkuu wa ranchi za Tiafa kwa kushindwa kuchukua hatua za kusimamia ujenzi wa mradi huo hadi kukamilika kwake.

Pia,waziri huyo wa kilimo ameagiza kupitia vyombo vya sheria,wahusika wote walioshiriki ama kwa makusudi au kwa njia yoyote kuhujumu mradi huo usifanikiwe wanachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo.

Mwisho, Nchemba amewaagiza wataalam wa wizara yake kuhakikisha ndani ya siku 7 wanampelekea ripoti ya thamani ya jengo lililokwisha kujengwa na fedha zinazotakiwa kumalizia ujenzi wa jengo hilo.

Sambamba na hatua hizo, Mwigulu ametoa rai kwa watumishi wote wa umma kuwa mstari wa mbele kusimamia kwa ufanisi na uzalendo miradi yote ya maendeleo ya nchi yetu,Mbali na hapo,serikali ya Magufuli haitakuwa tayari kuona mali ya umma inachezewa na kuibiwa wakati kuna watanzania wanaweza kusimamia mali hizo na kuziendeleza.

Picha/maelezo na Festo Sanga Jr

No comments:

Post a Comment