Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, January 13, 2016

NAIBU WAZIRI WA FEDHA DKT ASHATU KIJAJI AIAGIZA TRA MBEYA KUKUSANYA MAPATO KWA WABADILISHAJI WA FEDHA TUNDUMA

Naibu Waziri Fedha na Mipango Dkt,Ashatu Kijaji akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Mbeya  ( hawapo pichani)  mara baada ya kufanya ziara katika Mpaka wa Tunduma na Zambia .


Baadhi ya waandishi wa Habari Mkoani Mbeya wakiwa makini kumsikiliza Naibu waziri wa Fedha na Mipango Dkt Kishatu Kijaji katika ofisi za Mamlaka ya Mapato TRA Mkoani humo kwa lengo la kutoa tathimini yake ya ziara aliyoifanya katika Mpaka wa Tunduma na Zambia .

 
 Na Jamiimojablogu,Mbeya
Naibu waziri wa fedha na Mipango Dkt  Ashatu Kijaji ameitaka Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Mbeya kuhakikisha inaanda mpango maalumu kwa ajili kudhibiti mapato yanayopotea kutokana na kushamili kwa biashara ya ubadilishaji wa fedha kiholela katika mpaka wa Tunduma na Zambia.
Naibu waziri huyo ametoa kauli hiyo Mkoani Mbeya mara baada ya kutembelea Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani humo  na kutoa tathimini  ya ziara yake aliyoifanya katika Mpaka wa Tunduma na Zambia.
Amesema serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi hasa kutokana na kuwepo kwa biashara hiyo kiholela pasipo serikali kupata mapato yake hivyo  ameitaka mamlaka hiyo kuhakikisha inaweka mpango kabambe utakao iwezesha serikali kupata mapato yake kutokana na biashara hiyo.
Amesema serikali lazima ijiendeshe yenyewe kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato sanjali na kuzuia mianya yote ya ukwepaji wa kodi pamoja na watu wote kuhakikisha wanalipa kodi.
Amebainisha kuwa  nchi inategemea mapato kwa ajili ya kutoa huduma muhimu kwa wananchi na hivyo kuwaongezea wananchi matumaini kwa kuwafikishia huduma muhimu.
Sehemu nyingine ambayo ameiagiza mamlaka hiyo kuishughulikia mara moja  ili serikali iweze kupata mapato yake ni pamoja kuibuka kwa Saccos pamoja vikundi mbalimbali ambavyo vimekuwa vikijihusisha na ukopeshaji wa fedha kwa liba kubwa hali ambayo pia imekuwa ikiwapa mzigo mkubwa wananchi .
Katika hatua nyingine Naibu waziri huyo  ameuagiza uongozi wa mamlaka ya mapato (TRA) Katika mpaka wa Tunduma na Zambia kuhakikisha kuwa mizigo yote inayosafilishwa kupitia mpaka huo inafanyiwa tathimini na kulipiwa kwa muda wa usio zidi siku moja  tayari kuendelea na safari kwa inayoingia na kutoka nje ya Tanzania.
Ziara ya Naibu Waziri Dr. Kijaji ni ya kwanza Mkoani Mbeya  tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 11 Desemba 2015 kushika wadhifa huo.
Mwisho.

                  



No comments:

Post a Comment