skip to main |
skip to sidebar
TETESI ZA SOKA ULAYA -IJUMAA 29.01.2016
Chelsea wanamtaka meneja wa
Italy Antonio Conte, 46, awe meneja wa muda mrefu kuziba nafasi ya Jose
Mourinho (Mail), Manchester United wanamtaka mshambuliaji wa CSKA
Moscow, Ahmed Musa, 23, ambaye pia anasakwa na Leicester (Express), beki
wa Chelsea Gary Cahill anasakwa na Roma (London Evening Standard),
meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anafikiria kumsajili kiungo wa Udinese,
Pior Zielinski, 21 (Mirror), mshambuliaji wa Barcelona Neymar,
23, amesema angependa kucheza chini ya Pep Guardiola. Meneja huyo
anatarajiwa kwenda Manchester City mwisho wa msimu (Mirror), West Brom
wanazungumza na QPR kutaka kumsajili kwa mkopo kiungo wa zamani wa
Tottenham, Sandro (Telegraph), beki wa New York Red Bulls, Matt Miazga,
20, alikuwa London siku ya lhamisi ili kufanya vipimo vya afya Chelsea
(Sky Sports), dau la Arsenal la kumtaka Ben Chilwell, 19 kutoka
Leicester, limekataliwa (Football Insider), Newcastle United huenda
wakaacha kumfuatilia Saido Berahino, 22, licha ya kuwa tayari kutoa
zaidi ya pauni milioni 20, lakini West Brom wana 'dengua' (Newcastle
Chronicle), Newcastle huenda wakaamua
kumfuatilia Loic Remy, 29,
wakimkosa Berahino (Telegraph), West Ham na Norwich wanataka kumsajili
beki wa Inter Milan, Davide Santon, 25 kwa mkopo (Mail), uhamisho wa
kiungo wa West Ham Reece Oxford, 17, kwenda Charlton umekwama kwa sababu
meneja wa Charlton Jose Riga hajawahi kumsikia (Sun), mwekezaji
Mmarekani wa Bournemouth Matt Hulsizer, amesema meneja wake Eddie Howe
haendi popote. Howe, 38, amekuwa akihusishwa na kwenda Chelsea baada ya
Guus Hiddink kuondoka (Daily Echo), Manchester United wana matumaini ya
kumsajili kiungo kutoka Ureno, Domingos Quina, 16, anayeichezea Chelsea
(Sun), meneja wa Sunderland, Sam Allardyce amesema ana orodha ya majina
60 ya wachezaji anaowataka (Newcastle Chronicle), meneja wa Crystal
Palace, Alan Pardew ana wasiwasi kuwa Emmanuel Adebayor, 31, ataondoka
mwisho wa msimu (Star). Hayo ni baadhi ya yaliyoandikwa kwenye magazeti
ya Ulaya. Zimebaki siku tatu kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Siku njema!
No comments:
Post a Comment